-
Isaya 44:16, 17Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
16 Nusu yake huiteketeza motoni;
Kwa nusu hiyo huchoma nyama anayokula, naye hushiba.
Pia huota moto na kusema:
“Aha! Ninahisi joto ninapotazama moto.”
17 Lakini sehemu inayobaki anaifanya kuwa mungu, kuwa sanamu yake ya kuchongwa.
Anaiinamia na kuiabudu.
Anasali kwake na kusema:
“Niokoe, kwa maana wewe ni mungu wangu.”+
-
-
Danieli 3:5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 wakati mtakaposikia sauti ya pembe, zumari, zeze, kinubi cha pembe tatu, kinanda, zumari-tete, na ala nyingine zote za muziki, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza amesimamisha.
-