2 “Semeni jambo hili kati ya mataifa na mlitangaze.
Inueni ishara na mlitangaze.
Msifiche jambo lolote!
Semeni, ‘Babiloni ametekwa.+
Beli ameaibishwa.+
Merodaki ameshikwa na hofu.
Sanamu zake zimeaibishwa.
Sanamu zake zinazochukiza zimeshikwa na hofu.’