15 “Lakini msipoisikiliza sauti ya Yehova Mungu wenu kwa kuwa waangalifu kutenda amri zake zote na sheria zake ninazowaamuru leo, laana hizi zote zitawajia na kuwatangulia:+
29 Mtapapasa-papasa wakati wa adhuhuri, kama kipofu anavyopapasa-papasa gizani,+ nanyi hamtafanikiwa katika jambo lolote mnalofanya; na watu watawalaghai na kuwanyang’anya vitu vyenu daima, na hakuna atakayewaokoa.+