- 
	                        
            
            2 Wafalme 18:13, 14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
 - 
                            
- 
                                        
13 Katika mwaka wa 14 wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru+ alipanda kuja kuyashambulia majiji yote yenye ngome ya Yuda na kuyateka.+ 14 Kwa hiyo Mfalme Hezekia wa Yuda akatuma ujumbe huu kwa mfalme wa Ashuru kule Lakishi: “Nimekosea. Ondokeni, msinishambulie, nami nitalipa chochote mtakachonitoza.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Mfalme Hezekia wa Yuda faini ya talanta 300 za fedha* na talanta 30 za dhahabu.
 
 -