-
2 Wafalme 18:13, 14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
13 Katika mwaka wa 14 wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru+ alipanda kuja kuyashambulia majiji yote yenye ngome ya Yuda na kuyateka.+ 14 Kwa hiyo Mfalme Hezekia wa Yuda akatuma ujumbe huu kwa mfalme wa Ashuru kule Lakishi: “Nimekosea. Ondokeni, msinishambulie, nami nitalipa chochote mtakachonitoza.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Mfalme Hezekia wa Yuda faini ya talanta 300 za fedha* na talanta 30 za dhahabu.
-
-
2 Mambo ya Nyakati 28:19, 20Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Yehova aliwanyenyekeza watu wa Yuda kwa sababu ya Mfalme Ahazi wa Israeli, kwa maana aliwaacha watu wa Yuda watende watakavyo, na hivyo wakakosa kuwa waaminifu kwa Yehova kwa kiwango kikubwa.
20 Hatimaye Mfalme Tilgath-pilneseri+ wa Ashuru akaja kukabiliana naye na kumtesa+ badala ya kumtia nguvu.
-