-
2 Wafalme 25:4, 5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Sehemu ya ukuta wa jiji ilibomolewa,+ na wanajeshi wote wakakimbia wakati wa usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, wakati Wakaldayo walipokuwa wakilizingira jiji; naye mfalme akafuata njia inayoelekea Araba.+ 5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme, nalo likamfikia katika jangwa tambarare la Yeriko, na wanajeshi wake wote wakatawanyika na kumwacha.
-