15 “Lakini msipoisikiliza sauti ya Yehova Mungu wenu kwa kuwa waangalifu kutenda amri zake zote na sheria zake ninazowaamuru leo, laana hizi zote zitawajia na kuwatangulia:+
16 Mkivunja agano la Yehova Mungu wenu alilowaamuru mshike na mkienda kuabudu miungu mingine na kuiinamia, hasira ya Yehova itawaka dhidi yenu+ nanyi mtaangamia haraka kutoka katika nchi nzuri ambayo amewapa.”+