4 Wakuu wakamwambia mfalme: “Tafadhali agiza mtu huyu auawe,+ kwa maana hivyo ndivyo anavyoidhoofisha mioyo* ya wanajeshi waliobaki jijini, na pia ya watu wote, kwa kuwaambia maneno hayo. Kwa maana mtu huyu hawatakii amani watu hawa, bali msiba.”
6 Basi wakamchukua Yeremia na kumtupa ndani ya tangi la maji la Malkiya mwana wa mfalme, lililokuwa katika Ua wa Walinzi.+ Wakamshusha Yeremia ndani kwa kamba. Basi hapakuwa na maji ndani ya tangi hilo, ila matope tu, naye Yeremia akaanza kuzama ndani ya matope.