48 Yehova atawatuma maadui wenu wawashambulie, nanyi mtawatumikia+ mkiwa na njaa+ na kiu na uchi na mkiwa maskini kabisa.* Ataweka nira ya chuma kwenye shingo zenu mpaka atakapokuwa amewaangamiza.
19 Na wakiuliza, ‘Kwa nini Yehova Mungu wetu ametutendea mambo haya yote?’ mtawajibu, ‘Kama mlivyoniacha ili kumtumikia mungu wa kigeni katika nchi yenu, ndivyo mtakavyowatumikia wageni katika nchi isiyo yenu.’”+