-
1 Wafalme 7:9-12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Majengo hayo yote yalijengwa kwa mawe ghali+ yaliyochongwa kwa vipimo, yaliyokatwa ndani na nje kwa misumeno ya mawe, kuanzia kwenye msingi mpaka juu ya ukuta, na upande wa nje mpaka kwenye ule ua mkuu.+ 10 Na msingi ulijengwa kwa mawe makubwa sana na yaliyo ghali; baadhi ya mawe yalikuwa na ukubwa wa mikono kumi, na mawe mengine mikono minane. 11 Na juu ya mawe hayo kulikuwa na mawe ghali, yaliyochongwa kwa vipimo, na pia mbao za mierezi. 12 Ua mkuu ulizungukwa na ukuta wenye safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu ya maboriti ya mierezi, kama ulivyokuwa ua wa ndani+ wa nyumba ya Yehova na ukumbi wa nyumba.+
-