-
Kumbukumbu la Torati 28:54-57Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
54 “Hata mwanamume mpole sana na aliyedekezwa miongoni mwenu hatamhurumia ndugu yake au mke wake mpendwa au wanawe wanaobaki, 55 naye hatawagawia hata kidogo nyama ya wanawe ambayo atakula, kwa sababu hana kitu kingine chochote cha kula kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu katika majiji yenu.+ 56 Na mwanamke mpole sana na aliyedekezwa miongoni mwenu ambaye hata hawezi kuthubutu kukanyaga chini kwa wayo wa mguu wake kwa sababu ya kudekezwa sana+ hatamhurumia mume wake mpendwa wala mwanawe wala binti yake, 57 wala hata kondo la nyuma linalotoka katikati ya miguu yake wala wana anaozaa, kwa sababu atawala kwa siri kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu katika majiji yenu.
-