5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme, nalo likamfikia katika jangwa tambarare la Yeriko, na wanajeshi wake wote wakatawanyika na kumwacha. 6 Kisha wakamkamata mfalme+ na kumpeleka mpaka kwa mfalme wa Babiloni kule Ribla, nao wakamhukumu.
5 Lakini jeshi la Wakaldayo likawafuatia, nao wakamfikia Sedekia katika jangwa tambarare la Yeriko.+ Wakamkamata na kumleta kwa Mfalme Nebukadneza* wa Babiloni kule Ribla+ katika nchi ya Hamathi,+ ambako alimhukumu.