6 Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe waliobaki, Eleazari na Ithamari: “Msikose kutunza nywele zenu na msirarue mavazi yenu,+ msije mkafa na kumfanya Mungu awakasirikie Waisraeli wote. Ndugu zenu wote wa nyumba ya Israeli watawaombolezea wale ambao Yehova amewaangamiza kwa moto.