20 Sasa alikuwa amewakasirikia watu wa Tiro na Sidoni. Basi wakaja kwake wakiwa na kusudi moja, na baada ya kumshawishi Blasto, mwanamume aliyesimamia nyumba ya mfalme, wakatoa ombi la amani, kwa sababu nchi yao ilipata chakula kutoka kwa nchi ya mfalme.