-
Ufunuo 14:18-20Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
18 Na bado malaika mwingine akatokea katika madhabahu naye alikuwa na mamlaka juu ya moto. Naye akamwambia kwa sauti kubwa yule aliyekuwa na mundu mkali: “Tia ndani mundu wako mkali ukusanye vishada vya mzabibu wa dunia, kwa sababu zabibu zake zimeiva.”+ 19 Yule malaika akatia mundu wake katika dunia na kuukusanya mzabibu wa dunia, naye akautupa ndani ya shinikizo kubwa la divai la hasira ya Mungu.+ 20 Lile shinikizo la divai likakanyagiwa nje ya jiji, na damu ikatoka katika lile shinikizo la divai hata kufikia juu kwenye lijamu za farasi umbali wa stadia 1,600.*
-