-
Marko 7:25-30Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Mara moja mwanamke ambaye binti yake mdogo alikuwa na roho mwovu akasikia kumhusu Yesu, akaja na kuanguka miguuni pake.+ 26 Mwanamke huyo alikuwa Mgiriki, wa taifa la* Sirofoinike; naye aliendelea kumsihi sana Yesu amfukuze roho mwovu aliyekuwa ndani ya binti yake. 27 Lakini Yesu akamwambia: “Kwanza acha watoto washibe, kwa maana haifai kuchukua mkate wa watoto na kuwatupia mbwa wadogo.”+ 28 Hata hivyo, yule mwanamke akamjibu: “Ndiyo, bwana, lakini hao mbwa wadogo walio chini ya meza hula makombo ya watoto wadogo.” 29 Ndipo Yesu akamwambia: “Kwa sababu umesema hivyo, nenda; yule roho mwovu amemtoka binti yako.”+ 30 Basi akaenda nyumbani akamkuta yule mtoto akiwa amelala kitandani, na yule roho mwovu alikuwa amemtoka.+
-