Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 15:22-28
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 22 Na tazama! mwanamke fulani Mfoinike kutoka eneo hilo akamjia, akapaza sauti: “Nihurumie,* Bwana, Mwana wa Daudi. Binti yangu anasumbuliwa kikatili na roho mwovu.”+ 23 Lakini Yesu hakumjibu mwanamke huyo. Kwa hiyo wanafunzi wake wakaja na kumwambia: “Mwambie aende, kwa sababu anaendelea kutufuata akipaza sauti.” 24 Yesu akajibu: “Sikutumwa kwa yeyote isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.”+ 25 Lakini mwanamke huyo akaja na kumsujudia* akisema: “Bwana, nisaidie!” 26 Yesu akamjibu: “Haifai kuuchukua mkate wa watoto na kuwatupia mbwa wadogo.” 27 Mwanamke huyo akasema: “Ndiyo Bwana, lakini hata hao mbwa wadogo hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza ya mabwana wao.”+ 28 Ndipo Yesu akamwambia: “Ewe mwanamke, imani yako ni kubwa; na itendeke kama unavyotaka.” Na kuanzia saa hiyo binti yake akapona.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki