Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 8:1-9
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 8 Siku hizo umati mkubwa ukakusanyika tena, na hawakuwa na chakula. Basi, akawaita wanafunzi na kuwaambia: 2 “Ninausikitikia umati,+ kwa sababu tayari wamekaa pamoja nami siku tatu nao hawana chakula.+ 3 Nikiwaacha waende nyumbani wakiwa na njaa,* watazimia njiani, na baadhi yao wametoka mbali.” 4 Lakini wanafunzi wake wakamjibu: “Tutapata wapi mikate ya kuwatosha watu hawa mahali hapa pasipo na watu?” 5 Ndipo akawauliza: “Mna mikate mingapi?” Wakajibu: “Saba.”+ 6 Naye akauagiza umati uketi chini. Kisha akachukua ile mikate saba, akatoa shukrani, akaimega, na kuanza kuwapa wanafunzi wake waigawe, nao wakaugawia umati.+ 7 Walikuwa pia na samaki wachache wadogo, naye akawabariki, kisha akawaambia wawagawe hao pia. 8 Basi wakala wakashiba, kisha wakakusanya vipande vilivyobaki wakajaza vikapu saba vikubwa.+ 9 Kulikuwa na wanaume 4,000 hivi. Kisha Yesu akawaaga.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki