Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 15:32-38
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 32 Lakini Yesu akawaita wanafunzi wake na kuwaambia: “Ninausikitikia umati,+ kwa sababu tayari wamekaa pamoja nami siku tatu nao hawajala chochote. Sitaki kuwaacha waende wakiwa na njaa,* wasije wakazimia njiani.”+ 33 Hata hivyo, wanafunzi wakamwambia: “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuushibisha umati huu mkubwa mahali hapa pasipo na watu?”+ 34 Ndipo Yesu akawauliza: “Mna mikate mingapi?” Wakajibu: “Saba, na samaki wachache wadogo.” 35 Kwa hiyo, baada ya kuuagiza umati uketi chini, 36 akachukua ile mikate saba na wale samaki, na baada ya kutoa shukrani, akamega na kuanza kuwagawia wanafunzi, nao wanafunzi wakaugawia umati.+ 37 Na wote wakala wakashiba, kisha wakakusanya vipande vilivyobaki, wakajaza vikapu saba vikubwa.+ 38 Sasa wale waliokula walikuwa wanaume 4,000, na pia wanawake na watoto wadogo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki