-
Marko 8:13-21Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
13 Ndipo akawaacha, akapanda mashua tena na kuvuka ng’ambo ya bahari.
14 Hata hivyo, walisahau kuchukua mikate na walikuwa na mkate mmoja tu katika mashua.+ 15 Naye akawaonya waziwazi akisema: “Endeleeni kuwa macho; jihadharini na chachu* ya Mafarisayo na ya Herode.”+ 16 Basi wakaanza kubishana kati yao kwa sababu hawakuwa na mikate. 17 Yesu alipojua hilo, akawaambia: “Kwa nini mnabishana kuhusu kutokuwa na mikate? Je, bado hamjafahamu wala kuelewa? Je, bado mioyo yenu ni mizito isiweze kuelewa? 18 ‘Ingawa mna macho, kwa nini hamwoni; na ingawa mna masikio, kwa nini hamsikii?’ Je, hamkumbuki 19 nilipoimega ile mikate mitano+ kwa ajili ya wale wanaume 5,000, mlikusanya vipande vilivyobaki mkajaza vikapu vingapi?” Wakamwambia: “Kumi na viwili.”+ 20 “Nilipoimega ile mikate saba kwa ajili ya wale wanaume 4,000, mlikusanya vipande vilivyobaki mkajaza vikapu vikubwa vingapi?” Wakamwambia: “Saba.”+ 21 Ndipo akawauliza: “Je, bado hamjaelewa?”
-