-
Mathayo 16:5-12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Sasa wanafunzi wakavuka kwenda ng’ambo ya bahari lakini wakasahau kuchukua mikate.+ 6 Yesu akawaambia: “Muwe macho na mjihadhari na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”+ 7 Basi wakaanza kujadiliana, wakisema: “Hatukubeba mikate yoyote.” 8 Akijua hilo, Yesu akawauliza: “Ninyi wenye imani ndogo, kwa nini mnajadiliana kati yenu kuhusu kutokuwa na mikate? 9 Je, bado hamwelewi, au je, hamkumbuki ile mikate mitano kuhusiana na wale watu 5,000, na ni vikapu vingapi mlivyokusanya?+ 10 Au ile mikate saba kuhusiana na wale watu 4,000 na ni vikapu vingapi vikubwa mlivyokusanya?+ 11 Kwa nini hamwelewi kwamba sikuongea nanyi kuhusu mikate? Bali jihadharini na chachu* ya Mafarisayo na Masadukayo.”+ 12 Ndipo wakaelewa kwamba hakuwa akizungumza kuhusu chachu ya mikate, bali kujihadhari na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
-