-
Luka 15:3-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Ndipo akawaambia mfano huu: 4 “Ikiwa mmoja wenu ana kondoo 100, naye ampoteze mmoja, je, hatawaacha wale 99 nyikani aende kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate?+ 5 Na baada ya kumpata, anambeba mabegani na kushangilia. 6 Na anapofika nyumbani anawaita rafiki zake na jirani zake, na kuwaambia, ‘Shangilieni pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyekuwa amepotea.’+ 7 Vivyo hivyo, ninawaambia kwamba kutakuwa na shangwe nyingi mbinguni kwa sababu ya mtenda dhambi mmoja anayetubu+ kuliko kwa waadilifu 99 ambao hawahitaji kutubu.
-