16 “Aliyepotea nitamtafuta,+ anayetangatanga nitamrudisha, aliyejeruhiwa nitamfunga, na aliye dhaifu nitamtia nguvu; lakini aliyenona na aliye na nguvu nitamwangamiza. Huyo nitamlisha hukumu.”
12 “Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo 100 na mmoja apotee,+ je, hatawaacha wale 99 mlimani na kwenda kumtafuta yule aliyepotea?+13 Naye akimpata, hakika ninawaambia, yeye humshangilia huyo kuliko wale 99 ambao hawakupotea.