Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 12:18-23
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 18 Sasa Masadukayo, ambao husema hakuna ufufuo,+ wakaja na kumuuliza:+ 19 “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba mtu akifa na kuacha mke lakini hakuacha mtoto, ndugu yake anapaswa kumchukua mke huyo ili kumwinulia ndugu yake uzao.+ 20 Kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa mwanamke, lakini alipokufa hakuacha uzao wowote. 21 Wa pili akamwoa, lakini akafa bila kuacha uzao, na wa tatu vivyo hivyo. 22 Na wote saba hawakuacha uzao. Mwishowe pia yule mwanamke akafa. 23 Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Kwa maana wote saba walikuwa wamemwoa.”

  • Luka 20:27-33
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 27 Hata hivyo, baadhi ya Masadukayo, ambao husema hakuna ufufuo,+ wakaja na kumuuliza:+ 28 “Mwalimu, Musa alituandikia, ‘Ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke, lakini hakuwa na mtoto, ndugu yake anapaswa kumchukua mke huyo ili kumwinulia ndugu yake uzao.’+ 29 Basi kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa mwanamke lakini akafa bila mtoto. 30 Na wa pili 31 na wa tatu, wakamwoa mwanamke huyo. Vivyo hivyo wote saba; walikufa bila kupata watoto. 32 Mwishowe pia yule mwanamke akafa. 33 Kwa hiyo, katika ufufuo, atakuwa mke wa nani? Kwa maana wote saba walikuwa wamemwoa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki