-
Isaya 9:1, 2Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Hata hivyo, utusitusi huo hautakuwa kama nchi ilipokuwa na taabu, kama nyakati za zamani nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali zilipodharauliwa.+ Lakini baadaye Yeye ataifanya iheshimiwe—njia iliyo kando ya bahari, katika eneo la Yordani, Galilaya ya mataifa.
2 Watu waliokuwa wakitembea gizani
Wameona nuru kuu.
Na wale wanaokaa katika nchi ya kivuli kizito,
Nuru imewaangazia.+
-