-
Luka 8:35-37Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
35 Ndipo watu wakaenda kuona kilichotokea. Wakamjia Yesu na kumkuta yule mtu aliyetokwa na roho waovu ameketi miguuni pa Yesu, akiwa amevaa nguo na akiwa na akili timamu, nao wakaogopa. 36 Wale walioona jambo hilo wakawasimulia jinsi yule mtu aliyekuwa na roho waovu alivyoponywa. 37 Kisha watu wengi kutoka nchi ya Wagerasene wakamwomba Yesu aondoke, kwa sababu walikuwa wameogopa sana. Ndipo akapanda mashua ili aondoke.
-