Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 24:15-20
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 15 “Kwa hiyo, mtakapoona kile kitu chenye kuchukiza sana kinachosababisha ukiwa, kama alivyosema nabii Danieli, kikiwa kimesimama mahali patakatifu+ (msomaji na atumie utambuzi), 16 ndipo wale walio Yudea waanze kukimbilia milimani.+ 17 Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuchukua mali ndani ya nyumba yake; 18 na mtu aliye shambani asirudi kuchukua vazi lake la nje. 19 Ole wao wanawake wenye mimba na wale wanaonyonyesha mtoto katika siku hizo! 20 Endeleeni kusali ili mtakapokimbia isiwe wakati wa majira ya baridi kali wala siku ya Sabato;

  • Luka 21:20-23
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 20 “Hata hivyo, mtakapoona Yerusalemu limezingirwa na majeshi yaliyopiga kambi,+ jueni kwamba linakaribia kuharibiwa.+ 21 Ndipo wale walio Yudea waanze kukimbilia milimani,+ na wale walio Yerusalemu waondoke, nao wale walio mashambani wasiingie ndani yake, 22 kwa sababu hizi ni siku za kutekeleza haki,* ili mambo yote yaliyoandikwa yatimizwe. 23 Ole wao wanawake wenye mimba na wale wanaonyonyesha mtoto katika siku hizo!+ Kwa maana kutakuwa na mateso mengi katika nchi na ghadhabu dhidi ya watu hawa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki