-
Mathayo 26:42-46Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
42 Akaenda tena mara ya pili na kusali: “Baba yangu, ikiwa siwezi kuepuka kunywa kikombe hiki, acha mapenzi yako yatendeke.”+ 43 Akaja tena na kuwakuta wakiwa wamelala usingizi, kwa maana macho yao yalikuwa mazito. 44 Basi akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatu, akisema tena jambo lilelile. 45 Kisha akarudi na kuwaambia wanafunzi: “Mnalala na kupumzika wakati kama huu! Tazama! Saa imekaribia ya Mwana wa binadamu kusalitiwa mikononi mwa watenda dhambi. 46 Simameni twende. Tazama! Msaliti wangu amekaribia.”
-