-
Mathayo 27:11-14Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
11 Sasa Yesu akasimama mbele ya gavana, naye gavana akamuuliza: “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu: “Wewe mwenyewe umesema.”+ 12 Lakini alipokuwa akishtakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu.+ 13 Ndipo Pilato akamwambia: “Je, husikii ni mambo mangapi wanayoshuhudia dhidi yako?” 14 Lakini hakumjibu hata neno moja, hivi kwamba gavana akashangaa sana.
-