-
Mathayo 27:15-18Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Sasa kila sherehe ya pasaka, gavana alikuwa na desturi ya kumfungua mfungwa yeyote ambaye umati ulimtaka.+ 16 Wakati huo walikuwa wamemkamata mhalifu sugu aitwaye Baraba. 17 Basi walipokuwa wamekusanyika, Pilato akawauliza: “Mnataka niwafungulie nani, Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?” 18 Kwa maana Pilato alijua kwamba walikuwa wamemkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.
-