Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 17:17, 18
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 17 Yesu akajibu: “Enyi kizazi kisicho na imani na kilichopotoka,+ nitaendelea kuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa.” 18 Kisha Yesu akamkemea yule roho mwovu, naye akamtoka, na yule mvulana akapona kuanzia saa hiyo.+

  • Marko 9:19-27
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 19 Yesu akajibu: “Enyi kizazi kisicho na imani,+ nitaendelea kuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa.”+ 20 Basi wakamleta yule mvulana kwa Yesu, lakini yule roho mwovu alipomwona, mara moja akamfanya yule mtoto agaegae. Baada ya kuanguka chini, akaendelea kujiviringisha, akitoa povu mdomoni. 21 Yesu akamuuliza baba yake: “Jambo hili limekuwa likitokea kwa muda gani?” Akasema: “Tangu utotoni, 22 naye humwangusha ndani ya moto na ndani ya maji ili amuue. Lakini ikiwa unaweza kufanya chochote, tuhurumie na utusaidie.” 23 Yesu akamwambia: “Maneno hayo, ‘Ikiwa unaweza’! Mambo yote yanawezekana kwa mtu mwenye imani.”+ 24 Mara moja baba ya yule mtoto akasema kwa sauti kubwa: “Nina imani! Nisaidie mahali ambapo ninahitaji imani!”+

      25 Yesu alipoona umati ukikusanyika haraka, akamkemea yule roho mwovu, akamwambia: “Wewe roho bubu na kiziwi, ninakuagiza umtoke mtoto huyu na usimwingie tena!”+ 26 Baada ya kupaza sauti na kugaagaa sana, roho huyo akamtoka, na yule mtoto akaonekana ni kama amekufa, hivi kwamba watu wengi wakasema: “Amekufa!” 27 Lakini Yesu akamshika mkono na kumwinua, naye akasimama.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki