-
Mathayo 21:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Walipokaribia Yerusalemu na kufika Bethfage kwenye Mlima wa Mizeituni, Yesu akawatuma wanafunzi wawili,+ 2 akawaambia: “Nendeni katika kijiji mtakachokiona, na mara moja mtamwona punda amefungwa, na mwanapunda akiwa pamoja naye. Wafungueni na kuniletea. 3 Mtu yeyote akiwauliza, semeni, ‘Bwana anawahitaji.’ Na mara moja atawaruhusu mwachukue.”
-
-
Marko 11:1-6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
11 Walipokuwa wakikaribia Yerusalemu, Bethfage na Bethania+ kwenye Mlima wa Mizeituni, akawatuma wawili kati ya wanafunzi wake,+ 2 akawaambia: “Nendeni katika kijiji mtakachokiona, na mara tu mtakapoingia mtamwona mwanapunda akiwa amefungwa, ambaye hakuna mtu amewahi kuketi juu yake. Mfungueni na kumleta. 3 Mtu yeyote akiwauliza, ‘Kwa nini mnamfungua?’ mwambieni, ‘Bwana anamhitaji, na atamrudisha hapa mara moja.’” 4 Basi wakaenda na kumpata mwanapunda akiwa amefungwa kwenye mlango, karibu na barabara, nao wakamfungua.+ 5 Lakini watu waliokuwa wamesimama hapo wakawauliza: “Kwa nini mnamfungua mwanapunda huyu?” 6 Wakajibu kama Yesu alivyowaambia, nao wakawaacha waende.
-