-
Marko 11:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
11 Walipokuwa wakikaribia Yerusalemu, Bethfage na Bethania+ kwenye Mlima wa Mizeituni, akawatuma wawili kati ya wanafunzi wake,+ 2 akawaambia: “Nendeni katika kijiji mtakachokiona, na mara tu mtakapoingia mtamwona mwanapunda akiwa amefungwa, ambaye hakuna mtu amewahi kuketi juu yake. Mfungueni na kumleta. 3 Mtu yeyote akiwauliza, ‘Kwa nini mnamfungua?’ mwambieni, ‘Bwana anamhitaji, na atamrudisha hapa mara moja.’”
-
-
Luka 19:28-31Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
28 Baada ya Yesu kusema hayo, akapanda kuelekea Yerusalemu. 29 Alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye Mlima wa Mizeituni,+ akawatuma wawili kati ya wanafunzi,+ 30 akisema: Nendeni katika kijiji mtakachokiona, na mtakapoingia mtamwona mwanapunda akiwa amefungwa, ambaye hakuna mtu amewahi kuketi juu yake. Mfungueni na kumleta. 31 Lakini mtu akiwauliza, ‘Kwa nini mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.’”
-