-
Marko 14:13-16Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
13 Ndipo akawatuma wawili kati ya wanafunzi wake akawaambia: “Nendeni jijini, nanyi mtakutana na mwanamume akiwa amebeba mtungi wa maji. Mfuateni,+ 14 na popote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anasema: “Kiko wapi chumba cha wageni ambamo ninaweza kula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?”’ 15 Naye atawaonyesha chumba kikubwa cha juu, chenye vifaa na kilichotayarishwa. Tuandalieni humo.” 16 Basi wanafunzi wakaenda, wakaingia jijini na kupata kama alivyowaambia, nao wakaandaa Pasaka.
-