-
Mambo ya Walawi 12:6, 7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Siku zake za kujitakasa zitakapokwisha baada ya kuzaa mtoto wa kiume au wa kike, atamletea kuhani mwanakondoo dume wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu ya kuteketezwa+ na hua mchanga au njiwa tetere kwa ajili ya dhabihu ya dhambi kwenye mlango wa hema la mkutano. 7 Kuhani atatoa dhabihu hizo mbele za Yehova ili kufunika dhambi ya mwanamke huyo, kisha atakuwa safi kutokana na damu yake. Hiyo ndiyo sheria kuhusu mwanamke anayezaa mtoto wa kiume au wa kike.
-