-
Kutoka 26:31-33Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
31 “Utatengeneza pazia+ la nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, kitambaa cha rangi nyekundu, na kitani bora kilichosokotwa. Utalitarizi kwa michoro ya makerubi. 32 Utalining’iniza kwenye nguzo nne za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Kulabu zake zitakuwa za dhahabu. Nguzo hizo zitakaa juu ya vikalio vinne vya fedha. 33 Utalining’iniza pazia hilo chini ya vibanio na kuleta sanduku la Ushahidi+ humo, nyuma ya pazia. Pazia hilo litatenganisha Patakatifu+ na Patakatifu Zaidi.+
-