9 Mungu akaendelea kumwambia Abrahamu: “Wewe nawe, unapaswa kushika agano langu, wewe na uzao wako* baada yako katika vizazi vyao vyote. 10 Hili ndilo agano langu nililofanya pamoja nawe, ambalo wewe na uzao wako* baada yako mtalishika: Kila mwanamume miongoni mwenu ni lazima atahiriwe.+
48 Ikiwa mgeni anaishi pamoja nawe, naye anataka kusherehekea Pasaka ya Yehova, ni lazima kila mwanamume wa familia yake atahiriwe. Kisha anaweza kukaribia ili kuisherehekea, naye atakuwa kama mwenyeji wa nchi. Lakini mwanamume yeyote ambaye hajatahiriwa hapaswi kuila Pasaka.+
2 “Waambie Waisraeli, ‘Mwanamke akipata mimba na kuzaa mtoto wa kiume, mwanamke huyo hatakuwa safi kwa siku saba, atakuwa kama anavyokuwa katika siku zake za hedhi.+3 Siku ya nane, mtoto huyo atatahiriwa.+