-
Waamuzi 14:5, 6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Basi Samsoni akaenda na baba yake na mama yake hadi Timna. Alipofika katika mashamba ya mizabibu ya Timna, simba* akamjia akinguruma. 6 Ndipo roho ya Yehova ikamtia nguvu,+ naye akampasua simba huyo vipande viwili, kama mtu anavyompasua mwanambuzi kwa mikono yake. Lakini hakumwambia baba yake au mama yake jambo alilofanya.
-
-
1 Samweli 17:34-36Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
34 Ndipo Daudi akamwambia Sauli: “Mimi mtumishi wako nimekuwa nikichunga kondoo wa baba yangu, na simba+ akaja, na pia dubu, na kila mmoja wao akamchukua kondoo kutoka kundini. 35 Nilimfuata, nikamuua na kumwokoa kondoo kutoka kinywani mwake. Aliporuka ili kunishambulia, nilimkamata manyoya yake,* nikampiga, na kumuua. 36 Mimi mtumishi wako nilimuua simba na dubu pia, na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amevitukana* vikosi vya Mungu aliye hai.”+
-