19 “‘Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itawachukiza. Wala fedha yao wala dhahabu yao haitaweza kuwaokoa katika siku ya ghadhabu ya Yehova.+ Hawatashiba, wala kuyajaza matumbo yao, kwa maana vitu hivyo vimekuwa kikwazo kinachosababisha kosa lao.