Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • bi12 kur. 1966-1979
  • Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Vichwa vidogo
  • 1. Biblia
  • 2. Damu
  • 3. Dhambi
  • 4. Dini
  • 5. Dunia
  • 6. Fidia
  • 7. Har-magedoni
  • 8. Ibada ya Maria
  • 9. Ibilisi, Roho Waovu
  • 10. Kaburi (Hell, Hadesi, Sheoli)
  • 11. Kanisa
  • 12. Kifo
  • 13. Kuabudu Mababu wa Kale
  • 14. Kuandikiwa Kimbele Yatakayompata Mtu
  • 15. Kuchanganya Imani Mbalimbali
  • 16. Kuponya, Lugha
  • 17. Kurudi kwa Kristo
  • 18. Kutoa Ushahidi
  • 19. Manabii wa Uwongo
  • 20. Mashahidi wa Yehova
  • 21. Mbingu
  • 22. Mhudumu
  • 23. Mifano, Sanamu
  • 24. Msalaba
  • 25. Nafsi
  • 26. Ndoa
  • 27. Roho, Kuwasiliana na Pepo
  • 28. Sabato
  • 29. Sala
  • 30. Siku za Mwisho
  • 31. Sikukuu, Sikukuu za Kuzaliwa
  • 32. Tarehe za Matukio (Kronolojia)
  • 33. Ubatizo
  • 34. Ufalme
  • 35. Ufufuo
  • 36. Ukumbusho, Misa
  • 37. Uovu, Taabu za Ulimwengu
  • 38. Upinzani, Mateso
  • 39. Utatu
  • 40. Uumbaji
  • 41. Uzima
  • 42. Wokovu
  • 43. Yehova, Mungu
  • 44. Yesu
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia

Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia

1. Biblia

A. Neno la Mungu limeongozwa na roho

Wanadamu walichochewa na roho ya Mungu kuandika.  2Pe 1:20, 21

Ina unabii:  Da 8:5, 6, 20-22; Lu 21:5, 6, 20-22; Isa 45:1-4

Biblia nzima imeongozwa na roho ya Mungu na ina faida.  2Ti 3:16, 17; Ro 15:4

B. Ni mwongozo wenye kutumika kwa siku zetu

Kupuuza kanuni za Biblia kunaleta kifo.  Ro 1:28-32

Hekima ya binadamu haichukui nafasi ya Biblia.  1Ko 1:21, 25; 1Ti 6:20

Inatulinda na adui aliye na nguvu zaidi.  Efe 6:11, 12, 17

Humwongoza mwanadamu katika njia inayofaa.  Zb 119:105; 2Pe 1:19; Met 3:5, 6

C. Iliandikwa kwa ajili ya watu wa mataifa na jamii zote

Uandikaji wa Biblia ulianzia Mashariki.  Kut 17:14; 24:12, 16; 34:27

Uandalizi wa Mungu si kwa Wazungu tu.  Ro 10:11-13; Ga 3:28

Mungu hukubali watu wa namna zote.  Mdo 10:34, 35; Ro 5:18; Ufu 7:9, 10

2. Damu

A. Kutia damu mishipani huvunja utakatifu wa damu

Noa aliambiwa damu ni takatifu, ndiyo uhai.  Mwa 9:4, 16

Agano la Sheria lilikataza kula damu.  Law 17:14; 7:26, 27

Katazo hilo lilirudiwa kwa Wakristo.  Mdo 15:28, 29; 21:25

B. Suala la kuokoa uhai halifanyi iwe sawa kuvunja sheria ya Mungu

Utii ni bora kuliko dhabihu.  1Sa 15:22; Mk 12:33

Kutanguliza uhai wa mtu mwenyewe badala ya sheria ya Mungu kunaleta kifo.  Mk 8:35, 36

3. Dhambi

A. Maana ya dhambi

Kuvunja sheria ya Mungu, kiwango chake kikamilifu.  1Yo 3:4; 5:17

Mwanadamu, akiwa uumbaji wa Mungu, atatoa hesabu kwake.  Ro 14:12; 2:12-15

Sheria ilifafanua dhambi, ilifanya wanadamu waitambue.  Ga 3:19; Ro 3:20

Wote wana dhambi, wamepungukiwa na kiwango kikamilifu cha Mungu.  Ro 3:23; Zb 51:5

B. Sababu ya wote kupatwa na dhambi ya Adamu

Adamu alipitisha kutokamilika na kifo kwa wote.  Ro 5:12, 18

Mungu alikuwa mwenye rehema katika kuwavumilia wanadamu.  Zb 103:8, 10, 14, 17

Dhabihu ya Yesu hufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi.  1Yo 2:2

Dhambi na kazi nyingine zote za Ibilisi zitafutwa.  1Yo 3:8

C. Tunda lililokatazwa lilikuwa kutokutii, si tendo la ngono

Katazo la mti lilitolewa kabla ya kuumbwa kwa Hawa.  Mwa 2:17, 18

Adamu na Hawa waliambiwa wazae watoto.  Mwa 1:28

Watoto si tokeo la dhambi, bali ni baraka ya Mungu.  Zb 127:3-5

Hawa alitenda dhambi wakati mume hakuwapo; alijitanguliza.  Mwa 3:6; 1Ti 2:11-14

Adamu, akiwa kichwa, aliiasi sheria ya Mungu.  Ro 5:12, 19

D. Maana ya kuitendea dhambi roho takatifu (Mt 12:32; Mk 3:28, 29)

Dhambi ya kurithi si ya aina hiyo.  Ro 5:8, 12, 18; 1Yo 5:17

Huenda mtu akaihuzunisha roho, lakini apate nafuu.  Efe 4:30; Yak 5:19, 20

Kuzoea kufanya dhambi kwa kukusudia huongoza kwenye kifo.  1Yo 3:6-9

Mungu huwahukumu wanaofanya hivyo, huondoa roho yake.  Ebr 6:4-8

Hatupaswi kusali kwa ajili ya hao wasiotubu.  1Yo 5:16, 17

4. Dini

A. Kuna dini moja tu ya kweli

Tumaini moja, imani moja, ubatizo mmoja.  Efe 4:5, 13

Imepewa utume wa kufanya wanafunzi.  Mt 28:19; Mdo 8:12; 14:21

Inatambuliwa kwa matunda yake.  Mt 7:19, 20; Lu 6:43, 44; Yoh 15:8

Upendo, mapatano kati ya washiriki.  Yoh 13:35; 1Ko 1:10; 1Yo 4:20

B. Inafaa kushutumu mafundisho ya uwongo

Yesu alishutumu mafundisho ya uwongo.  Mt 23:15, 23, 24; 15:4-9

Alifanya hivyo ili kuwalinda waliopofushwa.  Mt 15:14

Kweli iliwaweka huru wawe wanafunzi wa Yesu.  Yoh 8:31, 32

C. Ni muhimu mtu kubadili dini ikithibitishwa kuwa ni ya uwongo

Kweli huweka mtu huru; huthibitisha kuwa wengi wamekosea.  Yoh 8:31, 32

Waisraeli, wengine, waliacha ibada ya kwanza.  Yos 24:15; 2Fa 5:17

Wakristo wa kwanza walibadili maoni.  Ga 1:13, 14; Mdo 3:17, 19

Paulo alibadili dini yake.  Mdo 26:4-6

Ulimwengu mzima umedanganywa, lazima mtu afanye upya akili yake.  Ufu 12:9; Ro 12:2

D. Unaoonekana kuwa “wema katika dini zote” hautoi uhakikisho wa kibali cha Mungu

Mungu huweka kiwango cha ibada.  Yoh 4:23, 24; Yak 1:27

Huo si wema kama haulingani na mapenzi ya Mungu.  Ro 10:2, 3

“Matendo mema” yaweza kukataliwa.  Mt 7:21-23

Hutambuliwa kwa matunda.  Mt 7:20

5. Dunia

A. Kusudi la Mungu kuelekea dunia

Paradiso ilifanywa duniani kwa ajili ya wanadamu wakamilifu.  Mwa 1:28; 2:8-15

Kusudi la Mungu ni hakika.  Isa 55:11; 46:10, 11

Dunia itajazwa wanadamu wenye amani, wakamilifu.  Zb 72:7; Isa 45:18; 9:6,7

Ufalme utairudisha Paradiso.  Mt 6:9, 10; Ufu 21:3-5

B. Haitaharibiwa kamwe wala kuondolewa wakaaji

Dunia halisi itadumu milele.  Mhu 1:4; Zb 104:5

Wanadamu wa wakati wa Noa waliharibiwa, si dunia.  2Pe 3:5-7; Mwa 7:23

Mfano huo watoa tumaini la kuokoka wakati wetu.  Mt 24:37-39

Waovu wataharibiwa; “umati mkubwa” utaokoka.  2Th 1:6-9; Ufu 7:9, 14

6. Fidia

A. Uhai wa kibinadamu wa Yesu ulilipwa kuwa “fidia kwa ajili ya wote”

Yesu alitoa uhai wake kuwa fidia.  Mt 20:28

Thamani ya damu iliyomwagwa huandaa msamaha wa dhambi.  Ebr 9:14, 22

Dhabihu moja ilitosha kwa wakati wote.  Ro 6:10; Ebr 9:26

Faida hazijileti tu; lazima zitambuliwe.  Yoh 3:16

B. Ilikuwa bei inayolingana

Adamu aliumbwa mkamilifu.  Kum 32:4; Mhu 7:29; Mwa 1:31

Kwa kutenda dhambi alijipotezea ukamilifu yeye na watoto wake.  Ro 5:12, 18

Watoto hawakuweza kujisaidia; mtu aliye sawa kabisa na Adamu alihitajiwa.  Zb 49:7; Kum 19:21

Uhai mkamilifu wa kibinadamu wa Yesu ni fidia.  1Ti 2:5, 6; 1Pe 1:18, 19

7. Har-magedoni

A. Vita vya Mungu vya kukomesha uovu

Mataifa yakusanywa kwenye Har-magedoni.  Ufu 16:14, 16

Mungu apigana, kwa kutumia Mwana na malaika.  2Th 1:6-9; Ufu 19:11-16

Jinsi tunavyoweza kuokoka.  Sef 2:2, 3; Ufu 7:14

B. Inapatana na upendo wa Mungu

Ulimwengu umeharibika sana.  2Ti 3:1-5

Mungu ana subira, lakini haki inataka hatua ichukuliwe.  2Pe 3:9, 15; Lu 18:7, 8

Lazima waovu waondoke ili waadilifu wasitawi.  Met 21:18; Ufu 11:18

8. Ibada ya Maria

A. Maria ni mama ya Yesu, si “mama ya Mungu”

Mungu hana mwanzo.  Zb 90:2; 1Ti 1:17

Maria alikuwa mama ya Mwana wa Mungu, katika hali yake ya kidunia.  Lu 1:35

B. Maria hakuwa “bikira sikuzote”

Aliolewa na Yosefu.  Mt 1:19, 20, 24, 25

Alikuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu.  Mt 13:55, 56; Lu 8:19-21

Hao wakati huo hawakuwa “ndugu zake wa kiroho.”  Yoh 7:3, 5

9. Ibilisi, Roho Waovu

A. Ibilisi ni mtu wa roho

Si uovu ulio ndani ya mtu mwenyewe bali ni mtu wa roho.  2Ti 2:26

Ibilisi ni mtu jinsi malaika walivyo.  Mt 4:1, 11; Ayu 1:6

Alijifanya Ibilisi kwa kuwa na tamaa mbaya.  Yak 1:13-15

B. Ibilisi ndiye mtawala asiyeonekana wa ulimwengu

Ulimwengu uko chini ya utawala wake akiwa mungu wake.  2Ko 4:4; 1Yo 5:19; Ufu 12:9

Ameruhusiwa kubaki mpaka suala litatuliwe.  Kut 9:16; Yoh 12:31

Atatiwa katika abiso, kisha aharibiwe.  Ufu 20:2, 3, 10

C. Roho waovu ni malaika waasi

Walijiunga na Shetani kabla ya Gharika.  Mwa 6:1, 2; 1Pe 3:19, 20

Walishushwa, wakatengwa na nuru yote.  2Pe 2:4; Yuda 6

Hupigana na Mungu, huwaonea wanadamu.  Lu 8:27-29; Ufu 16:13, 14

Wataharibiwa pamoja na Shetani.  Mt 25:41; Lu 8:31; Ufu 20:2, 3, 10

10. Kaburi (Hell, Hadesi, Sheoli)

A. Si mahali halisi penye moto wa mateso

Ayubu mwenye kutaabika alisali aende huko.  Ayu 14:13

Ni mahali pasipo na utendaji.  Zb 6:5; Mhu 9:10; Isa 38:18, 19

Yesu alifufuliwa kutoka kaburini, Hadesi.  Mdo 2:27, 31, 32; Zb 16:10

Kaburi litawatoa wengine waliokufa, litaharibiwa.  Ufu 20:13, 14

B. Moto ni mfano wa kuangamizwa

Moto hufananisha kukatiliwa mbali katika kifo.  Mt 25:41, 46; 13:30

Waovu wasiotubu waharibiwa milele kana kwamba kwa moto.  Ebr 10:26, 27

“Mateso” ya Shetani motoni ni kifo cha milele.  Ufu 20:10, 14, 15

C. Masimulizi ya tajiri na Lazaro si uthibitisho wa mateso ya milele

Moto si halisi kama vile kifua cha Abrahamu kisivyo halisi.  Lu 16:22-24

Kibali cha Abrahamu kinatofautishwa pia na giza.  Mt 8:11, 12

Kuangamizwa kwa Babiloni kunaitwa mateso ya moto.  Ufu 18:8-10, 21

11. Kanisa

A. Kanisa ni la kiroho, limejengwa juu ya Kristo

Mungu hakai katika mahekalu yaliyotengenezwa na mwanadamu.  Mdo 17:24, 25; 7:48

Kanisa la kweli ni hekalu la kiroho la mawe yaliyo hai.  1Pe 2:5, 6

Kristo ndiye jiwe la pembeni; mitume ni msingi wa pili.  Efe 2:20

Mungu anapasa kuabudiwa kwa roho na kweli.  Yoh 4:24

B. Kanisa halikujengwa juu ya Petro

Yesu hakusema kanisa limejengwa juu ya Petro.  Mt 16:18

Yesu atambulishwa kuwa ndiye “mwamba.”  1Ko 10:4

Petro alimtambulisha Yesu kuwa msingi.  1Pe 2:4, 6-8; Mdo 4:8-12

12. Kifo

A. Sababu ya kifo

Mwanadamu alikuwa na mwanzo mkamilifu, tazamio la uzima usio na mwisho.  Mwa 1:28, 31

Kutokutii kulileta hukumu ya kifo.  Mwa 2:16, 17; 3:17, 19

Dhambi na kifo vilipitishwa kwa watoto wote wa Adamu.  Ro 5:12

B. Hali ya wafu

Adamu alifanywa kuwa nafsi, hakupewa nafsi.  Mwa 2:7; 1Ko 15:45

Ni mwanadamu, nafsi, ambaye hufa.  Eze 18:4; Isa 53:12; Ayu 11:20

Wafu hawana fahamu, hawajui lolote.  Mhu 9:5, 10; Zb 146:3, 4

Wafu wamelala wakingojea ufufuo.  Yoh 11:11-14, 23-26; Mdo 7:60

C. Haiwezekani kuongea na wafu

Wafu hawako hai pamoja na Mungu wakiwa roho.  Zb 115:17; Isa 38:18

Tunaonywa juu ya kujaribu kusema na wafu.  Isa 8:19; Law 19:31

Wanaowasiliana na pepo, wapiga-ramli, hushutumiwa.  Kum 18:10-12; Ga 5:19-21

13. Kuabudu Mababu wa Kale

A. Kuabudu mababu wa kale ni ubatili

Mababu wa kale wamekufa, hawana fahamu.  Mhu 9:5, 10

Mababu wa kwanza hawastahili kuabudiwa.  Ro 5:12, 14; 1Ti 2:14

Mungu anakataza ibada hiyo.  Kut 34:14; Mt 4:10

B. Wanadamu wanaweza kuheshimiwa, lakini wa kuabudiwa ni Mungu tu

Vijana wanapaswa kuwaheshimu watu wenye umri mkubwa.  1Ti 5:1, 2, 17; Efe 6:1-3

Lakini ni Mungu tu anayepasa kuabudiwa.  Mdo 10:25, 26; Ufu 22:8, 9

14. Kuandikiwa Kimbele Yatakayompata Mtu

A. Binadamu hakuandikiwa kimbele yatakayompata

Kusudi la Mungu ni hakika.  Isa 55:11; Mwa 1:28

Watu mmoja-mmoja wamepewa uchaguzi wa kumtumikia Mungu.  Yoh 3:16; Flp 2:12

15. Kuchanganya Imani Mbalimbali

A. Kujiunga na dini nyingine si njia ya Mungu

Ni njia moja tu, ni nyembamba, ni wachache huipata.  Efe 4:4-6; Mt 7:13, 14

Tunaonywa kwamba mafundisho ya uwongo huchafua.  Mt 16:6, 12; Ga 5:9

Tunaamriwa kujitenga.  2Ti 3:5; 2Ko 6:14-17; Ufu 18:4

B. Si kweli kusema kuna “wema katika dini zote”

Nyingine zina bidii lakini si kupatana na Mungu.  Ro 10:2, 3

Ubaya huharibu mengine yote ambayo huenda yakawa mema.  1Ko 5:6; Mt 7:15-17

Walimu wa uwongo huleta uharibifu.  2Pe 2:1; Mt 12:30; 15:14

Ibada safi inataka mtu kujitoa kikamili.  Kum 6:5, 14, 15

16. Kuponya, Lugha

A. Kuponya kiroho kuna faida zenye kudumu

Ugonjwa wa kiroho unaharibu.  Isa 1:4-6; 6:10; Ho 4:6

Kuponya kiroho ndio utume wa msingi.  Yoh 6:63; Lu 4:18

Huondoa dhambi; huleta furaha, uzima.  Yak 5:19, 20; Ufu 7:14-17

B. Ufalme wa Mungu utaleta maponyo ya kimwili yenye kudumu

Yesu aliponya udhaifu mbalimbali, alihubiri baraka za Ufalme.  Mt 4:23

Ufalme umeahidiwa kuwa njia ya kuleta maponyo yenye kudumu.  Mt 6:10; Isa 9:7

Hata kifo kitafutiliwa mbali.  1Ko 15:25, 26; Ufu 21:4; 20:14

C. Uponyaji wa imani wa sasa hauna uthibitisho wa kibali cha Mungu

Wanafunzi hawakujiponya wenyewe kimuujiza.  2Ko 12:7-9; 1Ti 5:23

Zawadi za kimuujiza ziliisha baada ya siku za mitume.  1Ko 13:8-11

Kuponya si uthibitisho hakika wa kibali cha Mungu.  Mt 7:22, 23; 2Th 2:9-11

D. Kusema kwa lugha kulikuwa kuwe kwa muda mfupi tu

Kulikuwa ishara; zawadi kubwa zaidi zilipasa kutafutwa.  1Ko 14:22; 12:30, 31

Zawadi za kimuujiza za roho zilitabiriwa kupitilia mbali.  1Ko 13:8-10

Matendo ya ajabu si uthibitisho hakika wa kibali cha Mungu.  Mt 7:22, 23; 24:24

17. Kurudi kwa Kristo

A. Kurudi hakuonekani kwa wanadamu

Aliwaambia wanafunzi ulimwengu hautamwona tena.  Yoh 14:19

Ni wanafunzi tu walioona akipanda mbinguni; kurudi ni vivyo hivyo.  Mdo 1:6, 10, 11

Yuko mbinguni, ni roho asiyeonekana.  1Ti 6:14-16; Ebr 1:3

Anarudi katika nguvu za Ufalme wa mbinguni.  Da 7:13, 14

B. Hutambuliwa kwa mambo yanayoonekana

Wanafunzi waliuliza ishara ya kuwapo.  Mt 24:3

Wakristo “huona” kuwapo kwa njia ya uelewaji.  Efe 1:18

Matukio mengi ya pamoja ni uthibitisho wa kuwapo.  Lu 21:10, 11

Adui ‘huona’ uharibifu unapowafikia.  Ufu 1:7

18. Kutoa Ushahidi

A. Lazima Wakristo wote watoe ushahidi, watangaze habari njema

Lazima wamkiri Yesu mbele ya watu ili wakubaliwe.  Mt 10:32

Lazima kuwa mtendaji wa Neno, na kuonyesha imani.  Yak 1:22-24; 2:24

Wapya, pia, wapaswa kuwa walimu.  Mt 28:19, 20

Tangazo la hadharani huleta wokovu.  Ro 10:10

B. Uhitaji wa ziara za tena na tena, kuendelea kutoa ushahidi

Lazima onyo juu ya mwisho litolewe.  Mt 24:14

Yeremia alitangaza mwisho wa Yerusalemu kwa miaka mingi.  Yer 25:3

Kama vile Wakristo wa kwanza, hatuwezi kuacha.  Mdo 4:18-20; 5:28, 29

C. Lazima kutoa ushahidi ili tusiwe na hatia ya damu

Lazima kuonya juu ya mwisho unaokaribia.  Eze 33:7; Mt 24:14

Kutofanya hivyo huleta hatia ya damu.  Eze 33:8, 9; 3:18, 19

Paulo aliepuka hatia ya damu; alisema kweli kamili.  Mdo 20:26, 27; 1Ko 9:16

Humwokoa anayetoa ushahidi na pia yule anayesikiliza.  1Ti 4:16; 1Ko 9:22

19. Manabii wa Uwongo

A. Manabii wa uwongo walitabiriwa; walikuwako siku za mitume

Kanuni ya kutambua manabii wa uwongo.  Kum 18:20-22; Lu 6:26

Walitabiriwa; watambuliwa kwa matunda.  Mt 24:23-26; 7:15-23

20. Mashahidi wa Yehova

A. Mwanzo wa Mashahidi wa Yehova

Yehova hutambulisha mashahidi wake mwenyewe.  Isa 43:10-12; Yer 15:16

Mfuatano wa mashahidi waaminifu ulianza na Abeli.  Ebr 11:4, 39; 12:1

Yesu alikuwa shahidi mwaminifu na wa kweli.  Yoh 18:37; Ufu 1:5; 3:14

21. Mbingu

A. Ni 144,000 tu wanaoenda mbinguni

Hesabu yenye kikomo; watakuwa wafalme pamoja na Kristo.  Ufu 5:9, 10; 20:4

Yesu alikuwa mtangulizi; wengine wamechaguliwa tangu wakati huo.  Kol 1:18; 1Pe 2:21

Wengine wengi wataishi duniani.  Zb 72:8; Ufu 21:3, 4

144,000 katika cheo cha pekee ambacho wengine hawana.  Ufu 14:1, 3; 7:4, 9

22. Mhudumu

A. Wakristo wote lazima wawe wahudumu

Yesu alikuwa mhudumu wa Mungu.  Ro 15:8, 9; Mt 20:28

Wakristo hufuata kielelezo chake.  1Pe 2:21; 1Ko 11:1

Lazima wahubiri ili kutimiza huduma.  2Ti 4:2, 5; 1Ko 9:16

B. Sifa za kustahili kwa ajili ya huduma

Roho ya Mungu na ujuzi wa Neno lake.  2Ti 2:15; Isa 61:1-3

Fuata kielelezo cha Kristo katika kuhubiri.  1Pe 2:21; 2Ti 4:2, 5

Mungu huzoeza kwa kutumia roho, tengenezo.  Yoh 14:26; 2Ko 3:1-3

23. Mifano, Sanamu

A. Kutumia mifano, sanamu, katika ibada hushusha hadhi kwa Mungu

Haiwezekani kufanya sanamu ya Mungu.  1Yo 4:12; Isa 40:18; 46:5; Mdo 17:29

Wakristo wanaonywa juu ya sanamu.  1Ko 10:14; 1Yo 5:21

Mungu ni lazima aabudiwe kwa roho, kweli.  Yoh 4:24

B. Ibada ya sanamu ilileta kifo kwa taifa la Israeli

Wayahudi walikatazwa kuabudu sanamu.  Kut 20:4, 5

Haziwezi kusikia, kusema; wanaozitengeneza watakuwa kama hizo.  Zb 115:4-8

Zilileta mtego, uharibifu.  Zb 106:36, 40-42; Yer 22:8, 9

C. Ibada ya “kadiri” hairuhusiwi

Mungu alikataa kuruhusu ibada yake iwe ya “kadiri.”  Isa 42:8

Mungu peke yake ndiye “Msikiaji wa sala.” Zb 65:1, 2

24. Msalaba

A. Yesu alitundikwa juu ya mti wa kuulia iwe shutuma

Yesu alitundikwa juu ya mti au nguzo ya kuulia.  Mdo 5:30; 10:39; Ga 3:13

Wakristo ni lazima wauchukue mti kuwa shutuma.  Mt 10:38; Lu 9:23

B. Haupasi kuabudiwa

Kuonyesha mti wa Yesu ni shutuma.  Ebr 6:6; Mt 27:41, 42

Kutumia msalaba katika ibada ni kuabudu sanamu.  Kut 20:4, 5; Yer 10:3-5

Yesu ni roho, hayupo tena juu ya mti.  1Ti 3:16; 1Pe 3:18

25. Nafsi

A. Maana ya nafsi

Mwanadamu ni nafsi.  Mwa 2:7; 1Ko 15:45; Yos 11:11; Mdo 27:37

Wanyama huitwa nafsi pia.  Hes 31:28; Ufu 16:3; Law 24:18

Nafsi ina damu, hula, yaweza kufa.  Yer 2:34; Law 7:18; Eze 18:4

Mwanadamu, mwenye uhai, husemekana ana nafsi.  Mk 8:36; Yoh 10:15

B. Kuna tofauti kati ya nafsi na roho

Uhai ukiwa mtu au kiumbe ni nafsi.  Yoh 10:15; Law 17:11

Nguvu za uhai zinazotendesha nafsi huitwa “roho.”  Zb 146:4; 104:29

Mtu anapokufa, mamlaka juu ya nguvu za uhai hurudi kwa Mungu.  Mhu 12:7

Mungu tu ndiye anayeweza kutendesha nguvu za uhai.  Eze 37:12-14

26. Ndoa

A. Lazima muungano wa ndoa uheshimiwe

Yafananishwa na Kristo na bibi-arusi.  Efe 5:22, 23

Kitanda cha ndoa kisitiwe unajisi.  Ebr 13:4

Wenzi wa ndoa washauriwa wasitengane.  1Ko 7:10-16

Por·neiʹa ndio msingi pekee wa Kimaandiko wa talaka.  Mt 19:9

B. Kanuni ya ukichwa lazima iheshimiwe na Wakristo

Mume akiwa kichwa lazima aipende, aitunze familia.  Efe 5:23-31

Mke, hujitiisha, humpenda, humtii mume.  1Pe 3:1-7; Efe 5:22

Lazima watoto wawe watiifu.  Efe 6:1-3; Kol 3:20

C. Daraka la wazazi Wakristo kwa watoto

Lazima waonyeshe upendo, kutoa wakati, uangalifu.  Tit 2:4

Msiwakasirishe.  Kol 3:21

Toa mahitaji, kutia ndani mambo ya kiroho.  2Ko 12:14; 1Ti 5:8

Wape mazoezi ya maisha.  Efe 6:4; Met 22:6, 15; 23:13, 14

D. Wakristo wanapaswa kufunga ndoa na Wakristo tu

Funga ndoa “katika Bwana” tu.  1Ko 7:39; Kum 7:3, 4; Ne 13:26

E. Ndoa ya wake wengi si ya Kimaandiko

Mwanzoni mtu alipaswa kuwa na mke mmoja tu.  Mwa 2:18, 22-25

Yesu alirudisha kiwango kwa Wakristo.  Mt 19:3-9

Wakristo wa kwanza hawakuoa wake wengi.  1Ko 7:2, 12-16; Efe 5:28-31

27. Roho, Kuwasiliana na Pepo

A. Maana ya roho takatifu

Ni nguvu za utendaji za Mungu, si mtu.  Mdo 2:2, 3, 33; Yoh 14:17

Ilitumiwa katika uumbaji, kuongoza uandikaji wa Biblia, n.k.  Mwa 1:2; Eze 11:5

Huzaa, hutia mafuta, washiriki wa mwili wa Kristo.  Yoh 3:5-8; 2Ko 1:21, 22

Hutia nguvu, huongoza watu wa Mungu leo.  Ga 5:16, 18

B. Nguvu za uhai zinaitwa roho

Msingi wa uhai, hutegemezwa na kupumua.  Yak 2:26; Ayu 27:3

Mungu ndiye mwenye mamlaka juu ya nguvu za uhai.  Zek 12:1; Mhu 8:8

Nguvu za uhai za wanadamu, wanyama, ni mali ya Mungu.  Mhu 3:19-21

Roho hukabidhiwa Mungu kukiwa na tumaini la ufufuo.  Lu 23:46

C. Lazima kuwasiliana na pepo kuepukwe kwa kuwa ni kazi ya roho waovu

Neno la Mungu linakataza.  Isa 8:19, 20; Law 19:31; 20:6, 27

Upigaji-ramli ni ibada ya roho waovu; unashutumiwa.  Mdo 16:16-18

Huongoza kwenye uharibifu.  Ga 5:19-21; Ufu 21:8; 22:15

Unajimu unakatazwa.  Kum 18:10-12; Yer 10:2

28. Sabato

A. Siku ya Sabato si takwa kwa Wakristo

Sheria ilifutwa kwa msingi wa kifo cha Yesu.  Efe 2:15

Sabato si takwa kwa Wakristo.  Kol 2:16, 17; Ro 14:5, 10

Walikaripiwa kwa kushika Sabato, n.k.  Ga 4:9-11; Ro 10:2-4

Wanaingia pumziko la Mungu kwa imani na utiifu.  Ebr 4:9-11

B. Kushika Sabato kulitakiwa kwa Israeli wa kale tu

Sabato ilishikwa kwa mara ya kwanza baada ya Kutoka.  Kut 16:26, 27, 29, 30

Ilikuwa ishara ya pekee kwa Israeli wa asili.  Kut 31:16, 17; Zb 147:19, 20

Miaka ya Sabato pia ilikuwa takwa chini ya Sheria.  Kut 23:10, 11; Law 25:3, 4

Sabato si lazima kwa Wakristo.  Ro 14:5, 10; Ga 4:9-11

C. Pumziko la Mungu la Sabato (siku ya 7 ya “juma” la uumbaji)

Lilianza mwishoni mwa uumbaji duniani.  Mwa 2:2, 3; Ebr 4:3-5

Liliendelea hata baada ya siku za Yesu duniani.  Ebr 4:6-8; Zb 95:7-9, 11

Wakristo hupumzika kutokana na kazi za faida za kibinafsi.  Ebr 4:9, 10

Litamalizika Ufalme utakapokamilisha kazi kuelekea dunia.  1Ko 15:24, 28

29. Sala

A. Sala ambazo Mungu husikia

Mungu husikiliza sala za wanadamu.  Zb 145:18; 1Pe 3:12

Wasio waadilifu hawasikilizwi ila wabadili mwendo.  Isa 1:15-17

Lazima mtu asali katika jina la Yesu.  Yoh 14:13, 14; 2Ko 1:20

Lazima mtu asali kupatana na mapenzi ya Mungu.  1Yo 5:14, 15

Imani ni muhimu.  Yak 1:6-8

B. Sala zinazorudiwa-rudiwa bure kwa Maria au “watakatifu” hazifai

Lazima kusali kwa Mungu katika jina la Yesu.  Yoh 14:6, 14; 16:23, 24

Maneno ya kurudiwa-rudiwa hayatasikiwa.  Mt 6:7

30. Siku za Mwisho

A. Maana ya “mwisho wa ulimwengu”

Mwisho wa mfumo wa mambo.  Mt 24:3; 2Pe 3:5-7; Mk 13:4

Si mwisho wa dunia, bali wa mfumo mwovu.  1Yo 2:17

Wakati wa mwisho watangulia uharibifu.  Mt 24:14

Kuokoka kwa waadilifu; ulimwengu mpya utafuata.  2Pe 2:9; Ufu 7:14-17

B. Uhitaji wa kukaa macho kuelekea ishara za siku za mwisho

Ishara zinatolewa na Mungu ili kutuongoza.  2Ti 3:1-5; 1Th 5:1-4

Ulimwengu unashindwa kutambua uzito.  2Pe 3:3, 4, 7; Mt 24:39

Mungu hakawii, bali hutoa onyo.  2Pe 3:9

Thawabu ya kukaa macho, kujali.  Lu 21:34-36

31. Sikukuu, Sikukuu za Kuzaliwa

A. Sikukuu za kuzaliwa, Krismasi, hazikusherehekewa na Wakristo wa kwanza

Wale wasio waabudu wa kweli walisherehekea.  Mwa 40:20; Mt 14:6

Siku ya kifo cha Yesu kufanyiwa ukumbusho.  Lu 22:19, 20; 1Ko 11:25, 26

Sherehe za kupindukia hazifai.  Ro 13:13; Ga 5:21; 1Pe 4:3

32. Tarehe za Matukio (Kronolojia)

A. 1914 (W.K.) hukomesha Nyakati za Wasio Wayahudi

Mfuatano wa watawala wa ufalme wakatizwa, 607 K.W.K.  Eze 21:25-27

“Nyakati saba” kumalizika ndipo utawala urudishwe.  Da 4:32, 16, 17

Saba = 2 × nyakati 3 1⁄2, au 2 × siku 1,260.  Ufu 12:6, 14; 11:2, 3

Siku moja kwa mwaka mmoja. [Hufanya iwe miaka 2,520]  Eze 4:6; Hes 14:34

Kuendelea mpaka kusimamishwa kwa Ufalme.  Lu 21:24; Da 7:13, 14

33. Ubatizo

A. Ni takwa la Kikristo

Yesu aliweka kielelezo.  Mt 3:13-15; Ebr 10:7

Huonyesha kujikana au kujiweka wakfu.  Mt 16:24; 1Pe 3:21

Kwa wale tu wenye umri wa kutosha kufundishwa.  Mt 28:19, 20; Mdo 2:41

Uzamisho majini ndiyo njia inayofaa.  Mdo 8:38, 39; Yoh 3:23

B. Hauoshi dhambi

Yesu hakubatizwa ili kuosha dhambi.  1Pe 2:22; 3:18

Damu ya Yesu ndiyo huosha dhambi.  1Yo 1:7

34. Ufalme

A. Mambo ambayo Ufalme wa Mungu utawafanyia wanadamu

Kutimiza mapenzi ya Mungu.  Mt 6:9, 10; Zb 45:6; Ufu 4:11

Serikali yenye mfalme na sheria.  Isa 9:6, 7; 2:3; Zb 72:1, 8

Utaharibu uovu, utatawala dunia nzima.  Da 2:44; Zb 72:8

Utawala wa miaka 1,000 utaponya wanadamu, kurudisha Paradiso.  Ufu 21:2-4; 20:6

B. Utendaji waanza wakati adui za Kristo wangali wanatenda

Baada ya Kristo kufufuliwa alingojea muda mrefu.  Zb 110:1; Ebr 10:12, 13

Aanza kutawala, apigana na Shetani.  Zb 110:2; Ufu 12:7-9; Lu 10:18

Ufalme ulisimamishwa wakati huo, ole za dunia zinafuata.  Ufu 12:10, 12

Taabu ya sasa yamaanisha ni wakati wa kuunga mkono Ufalme.  Ufu 11:15-18

C. Haumo ‘katika mioyo,’ hausitawishwi kupitia jitihada za wanadamu

Ufalme uko mbinguni, si duniani.  2Ti 4:18; 1Ko 15:50; Zb 11:4

Haumo ‘katika mioyo’; Yesu alikuwa akizungumza na Mafarisayo.  Lu 17:20, 21

Si sehemu yoyote ya ulimwengu huu.  Yoh 18:36; Lu 4:5-8; Da 2:44

Utachukua mahali pa serikali na viwango vya ulimwengu.  Da 2:44

35. Ufufuo

A. Tumaini kwa wafu

Wote walio makaburini watafufuliwa.  Yoh 5:28, 29

Ufufuo wa Yesu ni uhakikisho kamili.  1Ko 15:20-22; Mdo 17:31

Watenda-dhambi juu ya roho hawatafufuliwa.  Mt 12:31, 32

Wale wanaoonyesha imani wamehakikishiwa hilo.  Yoh 11:25

B. Ufufuo kwenye uzima ama mbinguni au duniani

Wote hufa katika Adamu; hupokea uzima katika Yesu.  1Ko 15:20-22; Ro 5:19

Watakaofufuliwa watakuwa na maumbile tofauti.  1Ko 15:40, 42, 44

Wale walio pamoja na Yesu watakuwa kama yeye.  1Ko 15:49; Flp 3:20, 21

Wale wasiotawala watakuwa duniani.  Ufu 20:4b, 5, 13; 21:3, 4

36. Ukumbusho, Misa

A. Ukumbusho wa Mlo wa Jioni wa Bwana

Hufanywa mara moja kwa mwaka katika siku ya Pasaka.  Lu 22:1, 17-20; Kut 12:14

Ni kuadhimisha kifo cha kidhabihu cha Kristo.  1Ko 11:26; Mt 26:28

Wenye tumaini la mbinguni hushiriki kula.  Lu 22:29, 30; 12:32, 37

Jinsi mtu anavyojua ana tumaini hilo.  Ro 8:15-17

B. Misa si ya Kimaandiko

Msamaha wa dhambi hutaka damu imwagwe.  Ebr 9:22

Kristo ndiye Mpatanishi mmoja tu wa agano jipya.  1Ti 2:5, 6; Yoh 14:6

Kristo yuko mbinguni; hashushwi chini na kasisi.  Mdo 3:20, 21

Hakuna uhitaji wa kutoa tena dhabihu ya Kristo.  Ebr 9:24-26; 10:11-14

37. Uovu, Taabu za Ulimwengu

A. Anayesababisha taabu za ulimwengu

Utawala mwovu ni kisababishi cha nyakati mbaya leo.  Met 29:2; 28:28

Mtawala wa ulimwengu ni adui ya Mungu.  2Ko 4:4; 1Yo 5:19; Yoh 12:31

Ole zinaletwa na Ibilisi, wakati ni mfupi.  Ufu 12:9, 12

Ibilisi kufungwa, amani tukufu kufuata.  Ufu 20:1-3; 21:3, 4

B. Sababu ya uovu kuruhusiwa

Ibilisi alitilia shaka ushikamanifu wa viumbe kwa Mungu.  Ayu 1:11, 12

Waaminifu wamepewa nafasi ya kuthibitisha ushikamanifu.  Ro 9:17; Met 27:11

Ibilisi amethibitishwa kuwa mwongo, suala litasuluhishwa.  Yoh 12:31

Waaminifu watapewa thawabu ya uzima wa milele.  Ro 2:6, 7; Ufu 21:3-5

C. Wakati wa mwisho uliorefushwa ni uandalizi wenye rehema

Kama katika siku za Noa, huchukua muda kutoa onyo.  Mt 24:14, 37-39

Mungu hakawii, bali ni mwenye rehema.  2Pe 3:9; Isa 30:18

Biblia hutusaidia tusinaswe ghafula.  Lu 21:36; 1Th 5:4

Tafuta uandalizi wa Mungu sasa ili kupata ulinzi.  Isa 2:2-4; Sef 2:3

D. Suluhisho la taabu za ulimwengu si kutoka kwa wanadamu

Wanadamu wanahofu sana, wanafadhaika.  Lu 21:10, 11; 2Ti 3:1-5

Ufalme wa Mungu utafaulu, si wanadamu.  Da 2:44; Mt 6:10

Ili kuishi, fanya amani na Mfalme sasa.  Zb 2:9, 11, 12

38. Upinzani, Mateso

A. Sababu Wakristo wapingwa

Yesu alichukiwa, alitabiri upinzani.  Yoh 15:18-20; Mt 10:22

Kushikamana na kanuni za haki huhukumu ulimwengu.  1Pe 4:1, 4, 12, 13

Shetani, mungu wa mfumo huu, hupinga Ufalme.  2Ko 4:4; 1Pe 5:8

Mkristo haogopi, Mungu hutegemeza.  Ro 8:38, 39; Yak 4:8

B. Mke hapaswi kumruhusu mume amtenge na Mungu

Ilionywa kimbele; huenda wengine wakampa habari zisizo za kweli.  Mt 10:34-38; Mdo 28:22

Lazima mke amtegemee Mungu na Kristo.  Yoh 6:68; 17:3

Kwa uaminifu huenda akaokoa mume pia.  1Ko 7:16; 1Pe 3:1-6

Mume ni kichwa, lakini hapaswi kuamuru juu ya ibada.  1Ko 11:3; Mdo 5:29

C. Mume hapaswi kumruhusu mke amzuie asimtumikie Mungu

Lazima ampende mke na familia, atake wapate uzima.  1Ko 7:16

Ana daraka la kuamua, kutoa riziki.  1Ko 11:3; 1Ti 5:8

Mungu humpenda mwanamume anayetetea kweli.  Yak 1:12; 5:10, 11

Kukosa msimamo ili kuwe amani hufanya mtu akose kibali cha Mungu.  Ebr 10:38

Aongoze familia kwenye furaha katika ulimwengu mpya.  Ufu 21:3, 4

39. Utatu

A. Mungu, Baba, ni Mtu mmoja, mkuu zaidi katika ulimwengu mzima

Mungu si watu watatu.  Kum 6:4; Mal 2:10; Mk 10:18; Ro 3:29, 30

Mwana aliumbwa; Mungu alikuwa peke yake kabla ya hapo.  Ufu 3:14; Kol 1:15; Isa 44:6

Mungu ni mtawala wa ulimwengu mzima nyakati zote.  Flp 2:5, 6; Da 4:35

Mungu atainuliwa juu ya wote.  Flp 2:10, 11

B. Mwana ni mdogo kwa Baba kabla na baada ya kuja duniani

Mwana alikuwa mtiifu mbinguni, alitumwa na Baba.  Yoh 8:42; 12:49

Alikuwa mtiifu duniani, Baba ni mkuu zaidi.  Yoh 14:28; 5:19; Ebr 5:8

Amepandishwa cheo mbinguni, bado anajitiisha.  Flp 2:9; 1Ko 15:28; Mt 20:23

Yehova ni kichwa na Mungu wa Kristo.  1Ko 11:3; Yoh 20:17; Ufu 1:6

C. Umoja wa Mungu na Kristo

Sikuzote wana upatano kamili.  Yoh 8:28, 29; 14:10

Umoja, kama ule wa mume na mke.  Yoh 10:30; Mt 19:4-6

Waamini wote lazima wawe na umoja uleule.  Yoh 17:20-22; 1Ko 1:10

Ibada moja ya Yehova kupitia Kristo milele.  Yoh 4:23, 24

D. Roho takatifu ya Mungu ni nguvu zake za utendaji

Ni nguvu, si mtu.  Mt 3:16; Yoh 20:22; Mdo 2:4, 17, 33

Hiyo si mtu aliye mbinguni pamoja na Mungu na Kristo.  Mdo 7:55, 56; Ufu 7:10

Hiyo huelekezwa na Mungu ili kutimiza makusudi yake.  Zb 104:30; 1Ko 12:4-11

Wanaotumikia Mungu huipokea, huongozwa nayo.  1Ko 2:12, 13; Ga 5:16

40. Uumbaji

A. Wakubaliana na sayansi iliyothibitishwa; hukanusha mageuzi

Sayansi hukubaliana na utaratibu wa uumbaji.  Mwa 1:11, 12, 21, 24, 25

Sheria ya Mungu ya viumbe kuzaa kulingana na “aina” yake ni ya kweli.  Mwa 1:11, 12; Yak 3:12

B. Siku za uumbaji si siku za saa 24

“Siku” yaweza kumaanisha tu kipindi cha wakati.  Mwa 2:4

Siku moja kwa Mungu yaweza kuwa muda mrefu.  Zb 90:4; 2Pe 3:8

41. Uzima

A. Uzima wa milele umehakikishiwa wanadamu watiifu

Mungu, ambaye hawezi kusema uwongo, ameahidi uzima.  Tit 1:2; Yoh 10:27, 28

Uzima wa milele umehakikishiwa wale wanaoonyesha imani.  Yoh 11:25, 26

Kifo kitaharibiwa.  1Ko 15:26; Ufu 21:4; 20:14; Isa 25:8

B. Uzima wa mbinguni ni kwa wale tu walio ndani ya mwili wa Kristo

Mungu huchagua washiriki kama inavyompendeza.  Mt 20:23; 1Ko 12:18

Ni 144,000 tu wanaochukuliwa kutoka duniani.  Ufu 14:1, 4; 7:2-4; 5:9, 10

Hata Yohana Mbatizaji hatakuwa katika Ufalme wa mbinguni.  Mt 11:11

C. Uzima duniani umeahidiwa hesabu isiyo na kikomo, “kondoo wengine”

Hesabu iliyo na kikomo pamoja na Yesu mbinguni.  Ufu 14:1, 4; 7:2-4

“Kondoo wengine” si ndugu za Kristo.  Yoh 10:16; Mt 25:32, 40

Wengi sasa wanakusanyika kwa ajili ya wokovu duniani.  Ufu 7:9, 15-17

Wengine watafufuliwa kwa ajili ya uzima duniani.  Ufu 20:12; 21:4

42. Wokovu

A. Wokovu hutoka kwa Mungu kupitia dhabihu ya fidia ya Yesu

Uzima ni zawadi ya Mungu kupitia Mwana wake.  1Yo 4:9, 14; Ro 6:23

Wokovu unawezekana tu kupitia dhabihu ya Yesu.  Mdo 4:12

Matendo hayawezekani wakati wa “toba ya wakati wa kufa.”  Yak 2:14, 26

Lazima kujitahidi ili kuufikia.  Lu 13:23, 24; 1Ti 4:10

B. “Mtu akiisha kuokolewa, ameokolewa sikuzote” si wazo la Kimaandiko

Washiriki wa roho takatifu wanaweza kuanguka.  Ebr 6:4, 6; 1Ko 9:27

Waisraeli wengi waliharibiwa ingawa waliokolewa kutoka Misri.  Yuda 5

Wokovu si jambo la kutokea dakika moja.  Flp 2:12; 3:12-14; Mt 10:22

Wale wanaokengeuka wanakuwa wabaya zaidi kuliko hapo mwanzoni.  2Pe 2:20, 21

C. “Kuokolewa kwa watu wote ulimwenguni” si wazo la Kimaandiko

Toba haiwezekani kwa wengine.  Ebr 6:4-6

Mungu hapendezwi na kifo cha mwovu.  Eze 33:11; 18:32

Lakini upendo hauwezi kuendekeza ukosefu wa uadilifu.  Ebr 1:9

Waovu wataharibiwa.  Ebr 10:26-29; Ufu 20:7-15

43. Yehova, Mungu

A. Jina la Mungu

“Mungu” si jina la kibinafsi; Bwana wetu ana jina la kibinafsi.  1Ko 8:5, 6

Tunasali jina lake litakaswe.  Mt 6:9, 10

Jina la Mungu ni Yehova.  Zb 83:18; Kut 6:2, 3; 3:15; Isa 42:8

Jina katika Biblia ya Union Version ya Kiswahili.  Kut. 6:3; Zb 83:18; Isa 12:2; 26:4, n.k.

Yesu alijulisha jina hilo.  Yoh 17:6, 26; 5:43; 12:12, 13, 28

B. Kuwako kwa Mungu

Haiwezekani kumwona Mungu na kuishi.  Kut 33:20; Yoh 1:18; 1Yo 4:12

Si lazima kumwona Mungu ili kuamini.  Ebr 11:1; Ro 8:24, 25; 10:17

Mungu anajulikana kwa kazi zake zinazoonekana.  Ro 1:20; Zb 19:1, 2

Utimizo wa unabii unathibitisha kuwako kwa Mungu.  Isa 46:8-11

C. Sifa za Mungu

Mungu ni upendo.  1Yo 4:8, 16; Kut 34:6; 2Ko 13:11; Mik 7:18

Ana hekima kuu.  Ayu 12:13; Ro 11:33; 1Ko 2:7

Anatenda kwa haki.  Kum 32:4; Zb 37:28

Ni mweza-yote, ana nguvu zote.  Ayu 37:23; Ufu 7:12; 4:11

D. Si wote wanaomtumikia Mungu yule mmoja

Njia ambayo huonekana njema si yenye kufaa sikuzote.  Met 16:25; Mt 7:21

Barabara mbili, ni moja tu inayoongoza kwenye uzima.  Mt 7:13, 14; Kum 30:19

Miungu mingi lakini kuna Mungu mmoja tu wa kweli.  1Ko 8:5, 6; Zb 82:1

Kumjua Mungu wa kweli ni lazima ili kupata uzima.  Yoh 17:3; 1Yo 5:20

44. Yesu

A. Yesu ni Mwana wa Mungu na Mfalme aliyewekwa rasmi

Mzaliwa wa kwanza wa Mungu, alitumiwa kuumba vitu vingine vyote.  Ufu 3:14; Kol 1:15-17

Alifanywa kuwa mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, mdogo kidogo kuliko malaika.  Ga 4:4; Ebr 2:9

Alizaliwa kwa roho ya Mungu, akikusudiwa kuwa mbinguni.  Mt 3:16, 17

Alipandishwa kwenye cheo cha juu zaidi kuliko wakati wa maisha yake kabla ya kuwa mwanadamu.  Flp 2:9, 10

B. Imani katika Yesu Kristo ni ya lazima ili kupata wokovu

Kristo ndiye Uzao ulioahidiwa wa Abrahamu.  Mwa 22:18; Ga 3:16

Yesu tu ndiye Kuhani Mkuu, na fidia.  1Yo 2:1, 2; Ebr 7:25, 26; Mt 20:28

Uzima unapatikana kwa kumjua Mungu na Kristo, kutii.  Yoh 17:3; Mdo 4:12

C. Mengi zaidi ya imani katika Yesu yanahitajiwa

Imani ni lazima iambatane na matendo.  Yak 2:17-26; 1:22-25

Lazima kuzitii amri, kufanya kazi aliyofanya.  Yoh 14:12, 15; 1Yo 2:3

Si wote wanaotumia jina la Bwana watakaoingia katika Ufalme.  Mt 7:21-23

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki