“Zaeni Mkaongezeke”—Kiasi Gani?
●Maneno haya, “Zaeni mkaongezeke” yaliamriwa na Muumba kwa wanyama na wanadamu. (Mwa. 1:22, 28) Inajulikana kwamba kama kawaida miezi tisa hupita kati ya mtungo wa mimba na kuzaliwa kwa mwanadamu. Namna gani viumbe vingine vya dunia? Watu wengi wenye maarifa juu ya jambo hili hutoa vipindi vifuatavyo: vijidudu vidogo sana viitwavyo bacteria huzaana kuanzia dakika 20 mpaka siku kadha; kuku huagua vifaranga baada ya siku 21; vipanya huzaa baada ya siku 20 mpaka 21; bata, siku 23 mpaka 30; sungura, siku 30 mpaka 34; panya wa kufugwa (guinea pigs), siku 68 mpaka 71, nguruwe, siku 114; kondoo, siku 146; ng’ombe, siku 270; farasi, siku 330 mpaka 380; tembo (ndovu), siku 607 mpaka 641; nyangumi, siku 330 mpaka 550 (ikitegemea namna namna za mnyama huyo).
Kwa kawaida, jinsi aina ya kitu inavyozidi ukubwa, ndivyo muda wake wa kutungwa mimba mpaka kuzaa unavyokuwa mrefu zaidi.