Dawa ya Kale
Dr. Salvatore P. Lucia anaandika hivi katika kitabu Wine as Food and Medicine: “Matumizi ya divai kama dawa ya maambukizo mabaya yanayohusiana na mapafu yalianza zamani sana. Katika nyakati za kisasa imeonekana kuwa yenye kufaa sana katika kutibu mkamba [ugonjwa wa kifua] . . . na maambukizo mengine yanayohusiana ya mapafu. Divai yenye moto inashauriwa itumiwe wakati wa kupatwa na mafua na maambukizo mengine ya mapafuni. Mara nyingi ukitumia bilauri moja yenye divai wakati wa kulala kutazuia homa ya mafua kwa kuutia mwili jasho.” Na shauri la Biblia:
“Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.” “Tumia [divai] kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.”—Mit. 17:22; 1 Tim. 5:23.