Ukurasa wa Pili
Katika miongo michache iliyopita, binadamu amechagua mtindo-maisha ambao umetokeza uchafuzi mkubwa sana wa mazingira yenye uhai ya dunia—udongo, mito, bahari kuu, na halianga zimetiwa sumu. Kwa kweli tatizo hilo ni la kimataifa. Kama vile papa alivyotaarifu katika ujumbe wake kwa Siku ya Ulimwengu ya Amani (Januari 1, 1990): “Katika visa vingi athari za matatizo ya mazingira zimeruka mipaka ya Mataifa moja moja; hivyo utatuzi wazo hauwezi kupatikana kwa kiwango cha kitaifa tu.”—L’Osservatore Romano, Desemba 18-26, 1989.
Kutojali kwa binadamu juu ya wakati ujao wake ni kinyume cha hangaiko la Mungu kwa dunia, ambayo, hata hivyo, ni uumbaji wake na mali yake. (Isaya 45:18) Je! yawezekana kuwe na dunia safi? Ikiwa ndivyo, jinsi gani na wakati gani? Mfululizo wa makala za jalada letu wajibu maswali hayo.