Ukurasa wa Pili
“KARIBU sehemu moja ya tano ya wakaaji wa dunia ni vijana walio kati ya umri wa miaka 15 na 24.” Ndivyo lilivyoripoti UN Chronicle. Ilikadiriwa kwamba mwanzoni mwa mwongo huu mpya, idadi ya vijana ulimwenguni ilifikia kiwango cha elfu milioni moja! Leo vijana wanatazamisha sana—nguvu kubwa ya kukabiliana nayo.
Psychology Today liliripoti juu ya uchunguzi wa wabaleghe 6,000 katika mabara kumi tofauti. Ilipatikana kwamba zijapokuwa tofauti kubwa katika hali ya kiuchumi na kitamaduni, vijana huonyesha mitazamo na thamani ambazo “zafanana sana.” Kutokana na uchunguzi mbalimbali kama huo ufanani wa duniani pote wa vijana wa leo umetokea, na unachofunua huenda kikakustaajabisha.