Ukurasa wa Pili
SASA HIVI, sisi sote tuna shughuli tukifanyiza mali ambayo husogeza mbele biashara yao. Wewe unatengeneza kitu fulani ambacho wao wakitaka. “Wao” ni akina nani? Ni benki za damu na vitovu vyenye kukusanya plasma (umajimaji wa damu).
Watu wengi huamini kwamba shughuli ya damu hutaka kuokoa uhai tu. Lakini idadi inaongezeka ya wachambuzi wenye maoni mamoja ya kwamba uwekaji wa benki ya damu ni namna nyingine tu ya biashara kubwa. Basi, kwa kweli, chembe za damu huwa pesa.