Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 1/8 uku. 31
  • Gharika Yenye Uharibifu Mkubwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Gharika Yenye Uharibifu Mkubwa
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Upendo Waonyeshwa Kupitia Kazi Kubwa ya Kutoa Msaada
    Amkeni!—2002
  • Kitu Kisichoweza Kuharibiwa na Dhoruba
    Amkeni!—2003
  • Misaada Yatolewa Kotekote Duniani
    Amkeni!—2001
  • Kukua Pamoja Katika Upendo
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 1/8 uku. 31

Gharika Yenye Uharibifu Mkubwa

EBU WAZIA gharika inayogharikisha sehemu iliyo na ukubwa wa Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani zote pamoja. Basi, hayo ndiyo yaliyotukia mwaka jana katika Queensland, Australia. Charleville, mji ulio karibu na katikati ya sehemu iliyogharikishwa, ilibidi uhamwe. Wenyeji wapatao elfu tatu walisongamana katika mahema kwenye sehemu iliyoinuka katika uwanja wa ndege wa mahali hapo. Ikawa lazima wengine waokolewe kutoka juu za paa kwa kutumia helikopta.

Kikundi kidogo cha watu 35 kilichoshirikiana na Kundi la Charleville la Mashahidi wa Yehova kilitafuta kimbilio kwa Shahidi aliyeishi katika ardhi iliyo juu kilomita kumi nje ya mji. Hapa pakawa mahali pa msingi pa utendaji wa kusaidia wale walioachwa bila makao.

Kwa haraka, Mashahidi walianza kupeleka misaada. Katika Dalby, ulio umbali wa kilomita 550, kikundi cha wenye kujitolea kilianzishwa ili kusafisha nyumba zilizogharikishwa. Katika Roma, umbali wa kilomita 270 Mashahidi walikusanya chakula na vifaa vingine vya dharura, kama vile mablanketi na nguo. Baada ya kuchunguza sehemu hiyo kutoka hewani ili kuona uharibifu, wenye kujitoa walienda sehemu hiyo—zaidi ya mia moja.

Waliieleza sehemu hiyo ya msiba kuwa “isiyoweza kuwaziwa.” Tope la kunata na mchanga ulifunika kila kitu kwa kiasi cha sentimita tano. Vifaa vya nyumbani vilivyovunjika vilitapakaa katika vyumba, mazulia yaliharibiwa, vifaa vya stima vikalowa maji, magari yakapinduka. Harufu ya chakula chenye kuoza, mbao zenye maji, na takataka, ilijaa kila mahali.

Wenye kujitolea walianza kazi. Kufikia Jumamosi, Aprili 28, juma moja tu baada ya gharika, makao ya Mashahidi wa Charleville yalikuwa safi na yenye kustahika. Hata hivyo, si kusafisha tu kulikohitajiwa. Kikundi hicho cha kujitolea kilirudisha umeme kwenye makao na kutengeneza magari na vifaa vya nyumbani. Wenye kutandaza mazulia waliweka mazulia mapya; mafundi wa makabati walijenga na kuweka makabati mapya; maseremala, wapaka rangi, na mafundi wa mabomba walifanya kazi ya kutengeneza.

Tokeo: Majuma mawili baada ya gharika, Mashahidi wote walikuwa wamerudi katika makao yao yaliyotengenezwa. Hata hivyo, wajenzi hawakusaidia Mashahidi wenzao pekee. Wakati kikundi kimoja kiliposafisha makao ya Mkatoliki mmoja, alirudiarudia kuonyesha mshangao wake.

Katika Brisbane Mashahidi walisifiwa katika redio kwa ajili ya kazi yao baada ya gharika. Na katika Charleville, watu wengi wa mjini walishangaa kuona jinsi Mashahidi wanavyotenda kwa uharaka. Mtu mmoja ambaye hapo kwanza alikuwa amewapinga alisikika akisema hivi: “Na sisi huthubutu kuwafukuza milangoni mwetu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki