Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 6/8 uku. 24
  • Matokeo Mabaya ya Hasira

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matokeo Mabaya ya Hasira
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Hasira?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Hasira—Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Hasira
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Je! Ni Vibaya Nyakati Zote Kuwa na Hasira?
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 6/8 uku. 24

Matokeo Mabaya ya Hasira

JE! UNA mwelekeo wa hasira, tayari kuwakwa na ghadhabu kwa kasirisho dogo? Je! unachemka hasira na kukasirika kwa masiku, ukituliza roho ya kuumizwa mtu anapokuchukiza? Ikiwa ni hivyo, huenda ukawa unawaudhi zaidi wale walio karibu nawe; huenda ukawa unajiuwa kwa hasira.

Je! hasira kweli yaweza kufisha? Kulingana na ripoti ya karibuni kutoka The New York Times News Service, uwezekano si wa kukisiwa. Ripoti yaonyesha, kwa mfano, kwamba “hasira ya kuselelea ni yenye kuangamiza sana mwili hivi kwamba ni kama, au hata inazidi, uvutaji sigareti, unene kupita kiasi na mlo wa kunenepesha sana kama hatari kubwa sana ya kifo cha mapema.”

Kama ushuhuda, ripoti yataja baadhi ya uchunguzi wa kisayansi. Katika mmoja, wanafunzi kadhaa wa chuo kikuu wenye umri wa miaka 25 walipewa mitihani ya kiutu ili kupima kiwango cha hasira walizohisi katika hali za kila siku. Wachunguzi walifuatia wanafunzi hawa miaka 25 baadaye. Wale waliokuwa na kiwango kidogo cha hasira walikuwa na kiwango kidogo cha kifo. Ni asilimia 4 tu waliokufa wakiwa na umri wa miaka 50. Lakini wengi wenye hasira hawakuponyoka jinsi hiyo—asilimia 20 walikuwa wamekufa! Uchunguzi mwingine ulipata kwamba wale waliokuwa na kiwango cha hasira yote katika ujana baadaye walikuwa na kiwango kikubwa cha mafuta yapatikanayo katika damu yenye kudhuru maisha, yakiwaletea hatari kubwa ya ugonjwa wa moyo.

Namna gani wale ambao huchemka hasira polepole na tiisho la ghadhabu badala ya kutafuta njia yenye kufaa ya kushughulika na shida zao? Dakt. Mara Julius, tabibu wa epidemiolojia katika Chuo Kikuu cha Michigan, alichunguza kikundi cha wanawake kwa zaidi ya kipindi cha miaka 18. Alipata kwamba wale walioonyesha ishara za kuselelea, walikuwa na kiwango cha kifo mara tatu zaidi kuliko wale ambao hawakuwa na hasira kama hiyo. Yeye amalizia: “Kwa wanawake wengi, hasira yenye kudumu huonekana kuwa yenye hatari sana kwa kifo cha mapema kuliko uvutaji wa sigareti.”

Maelfu ya miaka kabla ya uchunguzi wowote wa kisayansi kama huo, Biblia ilionya juu ya hasira: “Jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka,” wasema mstari mmoja. (Waefeso 4:26) “Ukomeshe hasira, uache ghadhabu,” washauri mwingine. (Zaburi 37:8) Hata lenye kutokeza zaidi, Biblia iliunganisha kati ya hali yetu ya hisi na afya yetu ya kimwili ilipothibitisha: “Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili.”—Mithali 14:30.

[Picha katika ukurasa wa 24]

Mzishi aona mtu mwenye hasira na kutazamia kwa shangwe kupata “mteja”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki