Wale Hayawani wa Kifumbo wa Ufunuo
Je! wewe wajua maana ya hayawani huyu mwenye sura ya kiajabu na namba yake, 666? Ni nini maana ya wale hayawani wengine wa kitabu cha Biblia cha Ufunuo?
Hayawani hawa wa ufananisho hukuathiri wewe na ulimwengu mzima wa ainabinadamu. Jifunze maana yao. Soma kile kitabu chenye kurasa 320 Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! Utasisimuliwa na utambulisho ule wa wazi, wenye maelezo timamu juu ya hayawani hao, na pia drakoni, kahaba mkubwa, na wahusika wengine wa ufananisho wa Ufunuo. Kitabu hiki cha kusisimua chenye jalada gumu, chenye kurasa za ukubwa ulio sawa na gazeti hili, hutokeza ufikirio wa mstari kwa mstari wa kitabu kizima cha Biblia cha Ufunuo. Peleka maombi ya habari zaidi leo.
Tafadhali nipelekeeni habari kuhusu kitabu chenye kurasa 320 Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!