Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 12/8 kur. 3-4
  • Ainabinadamu Inatamani Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ainabinadamu Inatamani Ulimwengu Mpya
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ulimwengu Mpya wa Aina Gani?
  • Je! Wanadamu Wanaweza Kuleta Amani na Usalama Wenye Kudumu?
    Amani na Usalama wa Kweli—Wewe Unaweza Kuupataje?
  • Ulimwengu Mpya—Je! Utapata Kuja?
    Amkeni!—1993
  • Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004
  • Ni Nani Awezaye Kuleta Amani Yenye Kudumu?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 12/8 kur. 3-4

Ainabinadamu Inatamani Ulimwengu Mpya

ULIMWENGU mpya haujapata kutamaniwa sana kama ilivyo sasa. Miongo minane iliyopita ya vita, ghasia, njaa, tauni, uhalifu, na uchafuzi imekuwa na vituko vyenye kuogofya sana. Binadamu anataka kuamkia kwenye ulimwengu mpya wa amani. Wakiitikia tamaa hiyo, viongozi wa ulimwengu wameanza kusema kuhusu kubuni ulimwengu kama huo.

Bila shaka umepata kusikia au kusoma hotuba za watu mashuhuri wakipiga mbiu kwamba ulimwengu mpya u karibu. Rais wa U.S. George Bush alisema hivi katika hotuba katika Septemba 1991: “Usiku huu, ninapoona drama ya demokrasia ikifunuka kotekote tufeni, labda—labda tuko karibu zaidi na ulimwengu huo mpya kuliko wakati mwingine wowote.”

Viongozi wa ulimwengu wanaelekeza kwenye mwisho wa Vita Baridi kati ya mataifa ya Mashariki na mataifa ya Magharibi, kuwa ithibati kwamba ulimwengu mpya u karibu. Kwelikweli, ulimwengu unahisi kutulizwa kidogo wakati programu za kupunguza silaha zinapotekelezwa. Kupunguzwa kwa silaha za nyukilia kunatia nguvu tumaini la watu wengi la ulimwengu mpya wa amani na usalama.

Katika Aprili wa mwaka huu, George McGhee, aliyekuwa waziri msaidizi wa mambo ya serikali wakati wa uongozi wa rais wa U.S. John F. Kennedy aliyekufa, alijulisha hivi: “Sasa tuna nafasi—kwa kweli, jambo la lazima—ya kupanga mwongozo wa mfumo wa ulimwengu mpya unaotegemea mawazo mapya ya usalama.” Yeye aliongeza hivi: “Mimi naamini kwamba tumaini lenye nguvu zaidi kwa mfumo wa ulimwengu mpya wenye kufanikiwa, liko katika kuimarisha vifungo vya jumuiya ya kimataifa.”

McGhee alisema kwamba Ufaransa ilipoahirisha majaribio yayo ya nyukilia hadi mwisho wa 1992 hiyo ilikuwa “ni njia ya kushawishi mataifa mengine yenye uwezo wa nyukilia yafanye hivyohivyo.” Yeye pia alitaja kuhusu “jitihada [za Urusi] za kuchukua hatua ya kwanza kupunguza silaha za nyukilia na kuacha ule msimamo wa hatari wa kuwa tayari kwa vita vya nyukilia.”

Zaidi ya hayo, kwenye mkutano wa viongozi wa ulimwengu katika London katika Julai 1991, saba kati yao walijulisha kwamba muungano wa vita ya Ghuba ya Uajemi “ulihakikisha uwezo wa jumuiya ya kimataifa kutenda pamoja ‘ili kurejesha amani na usalama wa kimataifa na kutatua mahitilafiano.’”

Ulimwengu Mpya wa Aina Gani?

Yote hayo yanatia moyo. Lakini jiulize, Ni ulimwengu mpya wa aina gani ambao mataifa yanatumaini kuubuni? Je! ni ulimwengu usio na silaha na usio na vita?

McGhee ajibu hivi: “Ni lazima Amerika iweke uwezo wa silaha wa kutosha ili kuchangia sehemu yayo katika muungano wowote wa kijeshi wakati ujao, au ishinde iwapo vita haiepukiki.” Kwa hiyo viongozi wa ulimwengu hawatetei kuondolewa kwa silaha zote, wala hawaondolei mbali muungano wa kijeshi ikiwa “vita haiepukiki” kama McGhee alivyosema. Serikali haziwezi tu kuahidi ulimwengu mpya usio na vita. Kihalisi, zinajua kwamba haziwezi kubuni ulimwengu kama huo.

Kwa mfano, tazama yale ambayo tayari yametukia. Chini ya kichwa “Utaratibu wa Ulimwengu Mpya” katika New York Times, ya Mei 17, 1992, mwandikaji wa safu Anthony Lewis aliandika hivi: “Nilipotazama picha za televisheni za makombora yakiangukia [Sarajevo, Bosnia na Herzegovina,] na raia wakijikunyata kwa hofu, nilifikiri kwamba ustaarabu haukuwa umefanya maendeleo tangu mabomu ya Nazi yalipoangukia Rotterdam. Eti unaitwa utaratibu wa ulimwengu mpya.”

Na bado, zaidi ya kuondolewa kwa vita, kuna matatizo mengine mengi yanayohitaji kutatuliwa ili kubuni ulimwengu mpya wenye kuridhisha. Fikiria uchafuzi wenye kudhuru kisiri ambao polepole unaharibu hewa, ardhi, na bahari zetu; mashirika ya uhalifu yenye uwezo na mashirika ya biashara ya dawa za kulevya ambayo huwanyang’anya mamilioni ya watu mali na afya yao; uharibifu usiozuiwa wa misitu ya mvua ambao husababisha mmomonyoko wa udongo na hatimaye husababisha mafuriko yanayoharibu mimea.

Isitoshe, magonjwa mabaya ya kimwili bado yanangojea tiba, kutia na ugonjwa wa moyo, kansa, UKIMWI, leukemia, na kisukari. Na vipi kuhusu matatizo ya umaskini, ukosefu wa makao, upungufu wa chakula na maji, ukosefu wa lishe bora, kutojua kusoma na kuandika, na kuharibiwa kwa tabaka la ozoni? Kwelikweli, orodha hiyo yaendelea daima. Matatizo hayo makubwa ni kama rundo la mabomu yaliyotegwa. Ni lazima binadamu ayategue sasa kabla hayajalipuka katika mfululizo wa misiba inayoweza kusababisha kuangamia kwake. Je! yeye aweza kuanzisha ulimwengu mpya bila kuchelewa ili kufanya hivyo?

Kwa miaka mingi mashirika na wajumbe wa mikutano wamekuwa wakijitahidi kutatua matatizo ya dunia. Na bado, si kwamba matatizo hayo yameongezeka tu bali pia mengine mapya na yenye kutatanisha zaidi yamezuka. Je! kushindwa kwa mwanadamu kutatua hayo kwamaanisha kwamba tamaa ya ainabinadamu ya kupata ulimwengu mpya wenye usalama na amani, ni bure tu? Kwa uhakika tunaweza kujibu la! Tafadhali angalia kwa nini sisi tunasema hivyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki