Ukurasa wa Pili
KUNAJISIWA—Hofu Kuu ya Wanawake 3-11
Ni nini humsukuma mnajisi? Wanawake wanaweza kufanya nini ili kuepuka kunajisiwa? Ni nini kinachoweza kuwazuia wanaume wasiwe wanajisi? Maswali hayo na mengineyo yatajibiwa katika mfululizo wa makala za mwanzoni.
Je! Niende Kwenye Dansi ya Uhitimu? 20
Katika nchi fulani, kuhitimu shule ya upili hutia ndani kufanya karamu na kucheza dansi. Mara nyingi hiyo huongoza kwenye ukosefu wa adili na mambo mabaya hata zaidi. Mkristo mwenye kudhamiria apaswa aoneje dansi ya uhitimu?
Shimo Kubwa Zaidi Ulimwenguni Lililopata Kuchimbwa na Binadamu 23
Zuru shimo kubwa zaidi duniani lililopata kuchimbwa na binadamu, uchimbuzi mkubwa wa migodi ya shaba katika Bingham Picha kwa hisani ya Kennecott Utah Copper